KIJANA WA MIAKA 18 ALIYETAMBULIKA
KWA JINA LA JENI GODWIN MWAKALINGA MKAZI WA KIJIJI CHA MLOWO ALIKUTWA
AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI, TAYA LA KULIA,
MGONGONI, MKONO WA KUSHOTO PIA ALIKUWA AMECHINJWA SHINGO KISHA MWILI
WAKE KUTUPWA MBUGANI KARIBU NA MTO ICHESA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO
TAREHE 15.12.2014 MAJIRA YA SAA 08:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
ICHESA, KATA YA MYOVIZI, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO INADAIWA NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA
ALIYEKUWA MUME WA MAREHEMU AMBAYE AMEKAMATWA AITWAE ALOYCE MWASHILINDI
(20) MKAZI WA MLOWO KUENDELEA KUWA NA WIVU NAE KWA KUMTUHUMU MTALAKA
WAKE AMBAYE WALIACHANA MIEZI MITATU ILIYOPITA KUWA NA MAHUSIANO YA
KIMAPENZI NA WANAUME WENGINE.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALITOWEKA
NYUMBANI TAREHE 14.12.2014 JIONI NA KUONEKANA 15.12.2014 ASUBUHI AKIWA
AMEUAWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI
WILAYA MBOZI KWA UCHUNGUZI ZAIDI WA KITABIBU.
KATIKA TUKIO LA PILI:
WATU WATANO WAMEFARIKI DUNIA BAADA
YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.143 AJR AINA YA
MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ROBERT MWAKIBIBI (37)
MKAZI WA UYOLE KUACHA NJIA NA KISHA KUPINDUKA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA
KANTELA WILAYA YA RUNGWE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE
15.12.2014 MAJIRA YA SAA 11:45 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
KANTELA-NTOKELA, KATA YA NTOKELA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE,
MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.
WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI
WANAWAKE WATATU NA WANAUME WAWILI AMBAO NI 1. SOPHIA OMARY (50) MKAZI WA
MBALIZI 2. STELA MWALUSWASWA (38) MKAZI WA TUNDUMA 3. SUZANA MELELE
(31) MKAZI WA MBALIZI 4. BULELE MWAIPAJA (48) MKAZI WA UYOLE NA 5. JACOB
NYALUKE (17) MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI MBOZI MISHENI
NA MKAZI WA MBOZI.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 32
WALIJERUHIWA KATI YAO WANAUME NI 16 NA WANAWAKE NI 16 AMBAO WAMELAZWA
KATIKA HOSPITALI ZA MISHENI IGOGWE NA MAKANDANA – TUKUYU. CHANZO CHA
AJAIL NI HITILAFU KATIKA MFUMO WA BREKI WA GARI HILO. DEREVA ALIKIMBIA
MARA BAADA YA TUKIO NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment