……………………………………………………………………………..
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amewataka Mabalozi
wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali ulimwenguni
kuhakikisha kuwa wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwa
ni njia mojawapo ya kutekeleza diplomasia ya uchumi.
Waziri Membe aliyasema hayo wakati
akizindua zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro linalofanywa na mabalozi
mbalimbali wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi kwa lengo la kuutangaza
Mlima Kilimanjaro ili uweze kuvutia watalii wengi zaidi.
“Bado idadi ya watalii wanaofika
nchini kupanda mlima hairidhishi na jitihada kubwa zinahitajika kufanywa
na mabalozi kuhakikisha kuwa wanautangaza vema mlima kwa kuwa ni hazina
ya pekee tuliyonayo inayopaswa kuwa kitega uchumi kizuri kwa uchumi wan
chi yetu” alisema Membe.
Jumla ya mabalozi 14 wanashiriki
zoezi hili ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la
kuutangaza Mlima Kilimanjaro. Mabalozi hao ni pamoja na Adadi Rajabu
(Zimbabwe); Ramadhani Mwinyi (Umoja wa Mataifa); John Kijazi (India);
Batilda Burian (Kenya); Shamim Nyanduga (Msumbiji); Grace Mujuma
(Zambia); na Patrick Tsere (Malawi)
Wengine ni pamoja na Mbarouk Mbarouk (Saudi Arabia); Joseph
Sokoine (Mkurugenzi Bara la Amerika); Ladislaus Komba (Uganda); Azizi
Mlima (Malaysia); Radhia Msuya (Afrika Kusini); Daniel Ole Njoolay
(Nigeria) na Charles Sanga (Balozi mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya
Utalii )
No comments:
Post a Comment