TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 16, 2014

Moja ya Vifaa Hatari vya kivita Vinapotumika kwa Raia wasio na Makosa

Moja ya Vifaa Hatari vya kivita Vinapotumika kwa Raia wasio na Makosa
Na: Shaaban Mpalule
 
Mataifa mbali Mbali Duniani yamekuwa yakitengeneza Vifaa vyenye Sumu Kali kwa ajili ya Kutumia wakati wa Kupigana kati ya Jeshi na Majeshi ya Upinzani, kitendo ambacho mara nyingi kimekuwa kikileta madhala makuba kwa Jamii mbali mbali wasiokuwa na Hatia.

Kwa Vigezo hivyo vya kuwa na Siraha Kali imepelekea Mataifa yasiyokuwa na uwezo wa kumiliki Siraha hizo Kuwa watumwa wa Mataifa yenye Uwezo wa Kutengenza na Kumiliki Siraha hizo ambapo Suala la Kujikomboa kwa Mataifa haya Kutoka Mikononi mwa hayo Mataifa inaonekana kushindwa kutokana na mbinu zinazotumiwa na Mataifa Yenye nguvu katika kuyashurutisha Mataifa Dhaifu kufanya Matakwa kinyume na Haki Halali za Mataifa Yao.

Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo Tayari zimemezwa na huo udhaifu wa Kuyasujudia Mataifa Makubwa ilimokuwa wakati wa Ukoloni wakati huo wakitawaliwa kwa Bakora na Nguvu kazi tofauti na Miaka hii ambapo Watanzania wanaendelea kutawaliwa kwa kunyonywa haki zao pamoja na kudhohofishwa katika Uchumi wa Jamii kitendo kitakachosababisha mmomonyoko wa Imani hata kuvuruga Amani iliyopo kati ya Watawala, Watawaliwa na Wanyonyaji.

Viongozi mbali mbali wa Serikali(Watawala) Wazalendo na Wapigania haki za Tanzania, wakati wa Utawala huo walihakikisha kwamba Rasilimali zinakuwa ni Mali ya Jamii lengo ikiwa ni kutaka kulinda Haki za Raia katika kuwa na nguvu ya kujikomboa wenyewe na si kutegemea kukombolewa jambo linalokuja kuleta Madhala makubwa ya kushindwa kujikomboa pale unapotegemea Mkombozi kisha asiwe na Msaada tena kwako kwa wakati huo wa Dhiki na Maangaiko.

Lakini pia Serikali, ama Viongozi wa Serikali, wanaposhindwa kulinda haki na mali za Wanachi wao, Zikatapanywa na Kugawiwa kwa Watu ama Mataifa ya Mengine kwa Madai ya kubinafsishwa, ni sawa na Waandaaji wa Vifaa hatari na vyenye Sumu kali wanapokuwa wameandaa kwa ajili ya yale yatakayotokea wakati wa dhiki na njaa kwa Taifa.

Misingi Imara ya Utawala ni pamoja na kutoyumba Kiuchumi, kitendo ambacho kwa Tanzania ni Kitendawili kutokana na hali ya sasa kuwa ngumu kwa Wananchi wake na hivyo kuashiria dhahili jinsi uchumi wa Tanzania ulivyoyumba kutokana na Misingi ya Utawala uliopo kwa hivi sasa kutofuata Misingi ya haki za Binadamu na Utawala Bora.

Sheria ni Msumeno unakata huku na kule" tofauti na Sheria za Mataifa Mengine" ambapo Sheria ya Tanzania imekuwa ni kama Panga lisilokuwa na Makali, ambalo ukikata hata majani haliwezi kutokana na kuwa butu, kutokana na kwamba Tanzania sasa imeshindwa kusimamia Sheria zake kwa kushindwa kutekeleza Majukumu Muhimu yanayopaswa kutekelezwa kwa kufuatwa sheria inayoruhusu haki hizo kutekelezwa.

Sheria haiwezi kujitekeleza yenyewe bila kutekelezwa, na imewekwa ili itekelezwe kutokana na uwajibikaji wa Watu kisheria katika kazi na Majukumu katika Jamii, kwa kuwa haki ya Jamii ni katika kufuata Misingi ya Sheria Zilizowekwa kwa utaratibu wa Jamii husika.

Serikali ni Haki iliyowekwa na Watu ili kuitumikia Sheria iliyowekewa vipengele kwa lengo la kulinda haki za Wadogo na Wakubwa, Wanyonge na Wenye Nguvu, Maskini na Matajiri, Walemavu na Wasio, Vijana na Wazee, Wanawake na Wanaume, kwamba yeyote Miongoni mwa hao bila kujali alitumika kwa kiwango gani katika haki, hanapokiuka na kwenda kinyume cha Utaratibu wa Sheria Zilizowekwa aweze kuwajibishwa bila kuangalia ni Kiasi gani cha Mali alizonazo, Utajiri wake, Vyeo vyake, ama ametumika kwa kiasi gani katika Utumishi wake.

Na inapotokea Kiongozi wa aina yeyote, kushindwa kuwawajibisha Viongozi wa chini yake, kutokana na Makosa ya wazi wazi yanayoonekana yalitendwa na ama yametendwa, basi kiongozi huyo pia si Mwadilifu na wala hatendi haki kwa watu wake jamii inapaswa kuchukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kuweka Misimamo ya kutokuwa na Imani na baadhi ya Viongozi kama hao ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za haraka za Kufanya Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment