Airtel UNI255 UDSM yakata Utepe wa Michuano hiyo kwenye viwanja vya chuo kikuu .
Add caption |
Wachezaji
wa timu za Chuo cha Sayansi za Jamii (jezi nyeusi) na Chuo cha Uhandisi
na Teknolojia, wakigombea mpira wakati wa mchezo wa fainali ya
mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255,
yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi.
Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika
kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa. Kaimu
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda
akikagua wachezaji wa Chuo cha Sayansi za Jamii, kabla ya kuanza kwa
mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya
Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es
Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo,
uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa.
…………………………………………………………………………………………
Na: Mwandishi Wetu.
Fainali ya Mashindano ya
mpira wa miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
yanayojulikana kama Airtel UNI255 yaliyoshirikisha wanafunzi wote wa
schools na Colleges zilizopo chuoni hapo yamemalizika siku ya jumamosi
ya tarehe 13/12/2014 Katika Fainali iliyovikutanisha vyuo vya Sayansi ya
Jamii(College of Social Science)na Chuo cha Uhandisi na Teknolojia
(College of Engineering and Technology) ambapo hadi dakika tisini(90)
zinamalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)
zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Timu ya kitivo cha CoET
iliyokua na upinzani mkali kwa jumla ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata
bao dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Justin Rupia
kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa CoSS Chawaka Francis na
kumfanya mwamuzi wa mpambano huo Wema Ngota pamoja na wasaidizi wake
Benjamini Mbughi, Hellen Mduma, Iddi Mfaume, Ramadhan Pondamali,Jackison
Msilombo, Ally Sarehe na Faraji Gaibu,walioichezesha michezo hiyo tangu
tarehe 8 mwezi huu kuwa katika hali tete kutokana na shangwe, nderemo
na vifijo kutoka kwa Mashabiki wa CoET kucharuka uwanja mzima.
Kipindi cha Pili kila
timu ilifanya mabadiliko ambapo CoSS iliwatoa Emmanuel George na
Morrison Ng’owo na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji Rashidi Hussen na
Ramadhan Hussen dakika ya 67 na 75 huku wenzao wa kitivo cha CoET
aliingia mchezajji Tibe Mario kuchukua nafasi ya mchezaji George Michael
katika dakika ya 62 mabadiliko yaliyowanufaisha zaidi CoSS
waliposawazisha bao dakika za Majeruhi baada ya kutokea piga nikupige na
hivyo kuleta mtafaruku kutokana na Muda(Kiza) kuingia ambapo timu hizo
zilishindwa kupigiana Penalti ili kupata mshindi wa kwanza na mshindi wa
pili.
Katika michezo ya awali
timu hizo za College of Social Science waliokuwa kundi B lililokuwa
katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo Hostel
ilifanikiwa kuongoza vizuri ambapo ilicheza mechi 3 ikashinda moja na
kutoa sare ya bila kufungana mechi 2. matokeo yalioyowapa pointi 5 na
goli 2 na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali.
Katika michezo ya awali
timu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia-College of Engineering and
Technology(CoET) iliyokuwa kundi A lililokuwa katika viwanja vya chuo
kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) ilifanikiwa kuongoza pia vizuri na kupata
pointi zilizoiweka kwenye nafasi ya kucheza Fainali baada ya kushinda
hatua ya nusu fainali dhi ya timu ya UDBS.
Timu iliyochukua nafasi
ya tatu ni kitivo cha UDBS waliofanikiwa kuwafunga Kitivo cha SoED kwa
njia ya penalty baada ya kumaliza dakika 90 kwa kufungana 2-2 katika
mchezo uliokuwa wa upinzani mkubwa kutokana na timu ya SoED kuwa na
wachezaji wengi wakongwe waliokaa muda mrefu hapo chuoni na wameshiriki
michuano mingi na wamefanya vizuri na ndiyo timu pekee iliyokuwa ikipewa
nafasi kubwa ya kunyakua Uchampioni huo wa Chuo.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti timu Capateni wa Timu zilizoshiriki hatua ya nusu fainali,
Bodoo Oduon wa Timu ya CoET, Michezo hiyo imeleta changamoto kubwa kwa
wanafunzi na kuwataka wadhamini kujitokeza kudhamini michezo ya vyuo vya
mkoa wa Dar es Salaam.
“Tumefurahi pamoja,
tumecheza na kuruka ruka hii ni shangwe, tena mimi nasema hawa Airtel
hakika wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa, ni pesa ngapi wamewekeza hapa,
na hii ni kwa Chuo Kimoja tu ch UDSM na bado kuna hiyo michuano ya vyuo
vya Dar es Salaam, ni muunganiko mzuri unaoletwa na hawa Airtel kwa
kutuunganisha kati ya vyuo na vyuo”alisema Bodoo Oduon
Kuhusu kutopata matokeo
ya Mshindi wa kwanza timu kampteni wa CoSS Elias Mshomba alisema kuwa
ni kawaida kutokea jambo hilo, maana Fainali ilihusisha watoto wa baba
mmoja, kwamba jambo kubwa ni juu ya hizo College zilizoingia fainali
kuwa wawakilishi wa College Championship Dar es Salaam inayotazamiwa
kuunguruma mapema kuanzia mwezi wa tatu mwakani.
“Wewe unadhani kuna
jambo limeharibika hapa kwa kutopata mshindi wa kwanza ama wa pili, sisi
tulikuwa katika mchujo wa kupata wawakilishi wa chuo, kama ni zawadi
zote ni za UDSM, hivyo nawaomba wachezaji wote waliofanikiwa kuzifikisha
timu zao hatua ya nusu fainali, kuendelea na maandalizi makali ya
kuhakikisha tunatwaa hizo zawadi zinazokuja za ushindani wa vyuo vya Dar
es Salaam, mwenyewe umeona kiza kimeingia hivyo wachezaji wasingekuwa
na uwezo wa kumaliza penalty tano kabla ya usiku na hapa hakuna taa,
tusubiri hiyo michuano ambayo sijui wadhamini ni nani kama watakuwa ni
Airtel basi itakuwa Raha sana maana tumefurahishwa na Airtel” alisema
Elias Mshomba.
Akiongea kuhusiana na
mwenendo wa mashindano hayo kwa Waziri wa michezo wa jumuiya ya
wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam STANLRY JULIUS alisema
“Mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto wa kipekee hasa kutokana na
wadhamini wetu Airtel kutupatia vifaa vya kutosha na kwa namna moja
yameongeza hari sana kwa washiriki wote, na Pengine hii imekuwa ni
changamoto kwetu kutokana na Uwepo wa Michuano ya Wanavyuo, College
Championship Tanzania” alisema
Na kuongeza kuwa “sisi
kama UDSM tumepewa heshima kubwa ya kutoa wawakilishi wane watakaoungana
na College zingine Kuunda jumla ya Timu 32 za College Kanda ya
Mashariki,hivyo tumefaidika sana sisi kama chuo, kwa kuwa jambo lingine
tumeweza kufanya Selection (Usahili) wa kupata timu ya chuo (UDSM ALLY
STARS)ambayo inaweza kuwakilisha chuo kwenye michezo ya EAST AFRICAN
UNIVERSITIES COMPETITION, inayoshirikisha nchi za Afrika mashariki kwa
michezo ya Vyuo Vikuu,lakini pia nichukue Fulsa hii kuwaomba tena
Airtel, kupitia hii hii Airtel UNI255 kuweza kudhamini hatua inayofuata
ya Michezo ya Vyuo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, NACTE & Inter College
Championship-Dar es Salaam,itakayoshirikisha jumla ya vyuo 32, Kama
ulivyoona mwenyewe jinsi ushindani ulivyomkubwa na hata soka lenyewe
lipo vyuoni,shamra shamra zote hizi hapa ni chuo kimoja je itakapokuwa
imekutanisha vyuo vingine kama vile IFM,DIT,NIT,TRA,ISW,IAE,BANDARI
COLLEGE,CBE, DACICO, HEDEN HILL, NJUWENI, MUHIMBILI MEDICAL SCHOOLS,
KIBAHA COTC na St. JOSEPH UNIVERSITY ambazo tayari zimefuzu hatua ya
Makundi yake ya Michuano ya Bonanza la NACTE INTER COLLEGE DAR ES SALAAM
BONANZA unadhani shamra shamra zitakuwaje, na tunaomba hiyo Fainali ya
College za Dar es Salaam ifanyike Uwanja wa Taifa ili TFF na Makocha wa
Timu ya Taifa waje wachague wachezaji watakaoisaidia Tanzania katika
michuano ya Taifa na kimataifa”alisema STANLRY
Timu iliyoonyesha
nidhamu na Ushindani mkubwa wa kuwania hizo nafasi wakati wa mchujo huo
wa College ya UDSM ili kuingia kwenye ushiriki wa michuano ya Vyuo vya
Dar es Salaam ni SJMC iliyokuwa kinara wa kundi A katika viwanja vya
ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaa ni (School of Journalism and Mass
Communication) ilicheza mechi mbili na kushinda zote na kujitengenezea
pointi 6 na huku akiongoza kwa kuwa na bao 5 za kufunga.
Akizungumzia michezo
hiyo kwa upande wa College za UDSM mratibu wa College za chuo hicho
bwana. Albert Kimaro alisema kuwa “ Kundi B ambalo mechi zake
zilichezewa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo
Hostel, ndilo lililokuwa na timu zenye wachezaji wakongwe na liliongozwa
na COSS (College of Social Science) timu iliyokuwa na mashabiki wengi
na ambayo imeweza kucheza Fainali, lakini pia ndani ya UDSM zimeshiriki
College kama CONAS, ambayo pia ilikuwa na wachezaji wazuri, UDSL, COET,
COICT,ISK,na COHU” alisema Albert.
Mgeni Rasmi katika
Fainali hiyo Profesa Mapunda Mapunda baada ya ukaguzi wa wachezaji
aliwaasa kuwa na utulivu, Upendo, mshikamano, wakati wote wa michezo na
waepuke ugomvi wakati wote kwani michezo ujenga na kuimarisha mahusiano
mwao.
“kikubwa hapa ni jinsi
ya kujenga misingi imara ya michezo ndani ya vyuo vyetu, sina maana
katika chuo hiki pekee, bali vyuo vyetu vyote, lakini pia niseme kwamba
miaka ya nyumba hatukuwa na hamasa ya michezo vyuoni kutokana na miundo
mbinu, lakini wakati huu nadhani kwamba michezo ama vipaji vipo vingi
vyuoni, nimesikia kuna kampuni ya MIDETA entertainment imeanza harakati
za kuanzisha hii michezo ya vyuo vyote vya Dar es Salaam na Tanzania kwa
ujumla,inayojulikana kama College Championship Dar es Salaam, ambapo
kwa sasa kuna mtowano mwingine unaendelea wa vyuo vingine kupitia mfumo
uliowekwa wa Bonanza la Nacte inter College Dar Es Salaam ili kupata
timu zitakazoshiriki ligi hiyo itakayokuwa na timu 32, nina hakika
kwamba michuano itakuwa mizuri na itapendwa sana na pia itazalisha
vijana wengi watakaokuwa wasomi kasha wawakilishi wetu kimichezo”
alisema Profesa Mapunda.
Naye Meneja Uhusiano wa
Airtel Jackison Mbando alisema kuwa kuwa Mashindano yalikuwa mazuri na
timu na kwamba imewapa changamoto ya kuongeza udhamini kwenye michezo ya
vyuo, “ kama unavyoona mwenye jinsi Fainali ilivyosheheni watu utadhani
mechi yay a Mtani Jembe, upinzani ni mkubwa sana na imeleta changamoto
sana, lakini kubwa ni kuhakikisha kwamba Airtel inawafikia Watu wote kwa
namna ya pekee,
Tupo katika harakati za
kuboresha maisha ya wanavyuo kwani tunatambua kwamba wanahitaji kusoma
kwa kutumia Mitandao katika ulimwengu huu wa sasa ambao Airtel kama
unavyoona ni zaidi ya mitandao mingine, tunaanza sisi kisha wanafuata
wengine nah ii tumeanza kwa kuwa karibu na wanavyuo ili tuwape nafuu
katika usomaji na upataji wa mawasiliano, lakini si hivyo tu kama
unavyoona hapa leo mambo yamenoga katika kuwapa pia afya wanafunzi wa
vyuo kwani Michezo inaleta afya ndiyo maana tumeamua kuingia sasa
kusaidia na kudhamini hii michezo ya Vyuo, na sasa tumeanza na College
za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tunatarajia kufanya mazungumzo na
waandaaji wa Michezo ya vyuo kwa Mkoa wa Dar es Salaam (MIDETA
entertainment) tupate mahitaji yao tuangalie, uwezekano upo wao waje
tuzungumze na ikibidi hata kupata timu bora ya College za
Tanzania,(College Championship Tanzania”alisema Jackison Mbando.
Aidha katika kilele cha
tamasha hilo Airtel ilizindua kwa wanafunzi wa chuo kikuu huduma ya
UNI255 itakayowawezesha kuwasiliana , kuperuzi internet kwa gharama
nafuu.
No comments:
Post a Comment