Na Mwandishi Wetu.
Wadau wa Elimu ndani na nje ya
nchi wamejiandikisha kwa wingi tayari kwa kushiriki maonesho ya kwanza
ya kimataifa ya elimu nchini ambayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania,
pamoja na kampuni ya uwakala wa vyuo vya nje Global Education link.
Maonesho hayo yanatarajiwa kuwa
ya aina yake kuwahi kutokea nchini yanawashiriki kutoka shule za msingi
na sekondari za serikali na binafsi,Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya
nchi,Asasi za kielimu za ndani na nje ya nchi ambazo huto udhamini kwa
wanafunzi.
Katika maonesho hayo kutakuwa na
banda maalum la Watanzania wataalam wanaosoma nje ya nchi katika fani
za sayansi na teknolojia hasa masomo ya gesi na mafuta ambao watatumia
fusra hiyo kutoa ushauri na elimu zaidi namna nchi zilizoendelea
zinavyotumia fusra hizo pamoja na kuwashauri vijana wakitanzania
ilikuweza kupata elimu sahihi hasa kwenye masuala mtambuka kama gesi na
mafuta ambazo zimegunduliwa nchini Tanzania.
Mratibu wa maonesho hayo
mkurugenzi mtendaji wa Global Education Link ,Abdulmalik Mollel
(Pichani) amesema hii itakuwa fusra ya kipekee wa vyuo vya elimu ya juu
hapa nchini kutoa maelezo ya kina kwa kozi pamoja huduma wanazotoa
ilikujenga uelewa sahihi kwa wazazi,wanafunzi wa sasa pamoja na
wanafunzi ambao wanatarajiwa kujiunga vyuo vikuu hivi karibuni.
Tume ya vyuo vikuu TCU watakuwa
sehemu ya wadau muhimu wa elimu ambao watatumia maonesho hayo kutoa
maelezo kwa wanafunzi waliohitimu ngazi mbalimbali ambao wanatarajia
kujiunga vyuo vikuu hasa namna ya kufuata taratibu za kuomba udahili kwa
umakini bila kukiuka taratibu.
Maonesho hayo ambayo yamebeba
kauli mbiu ‘KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU
TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA.’
Yatashirikisha wadau wanaotoa huduma za elimu kama vile wanaouza vifaa
vya elimu sare za shule na vyuo,vifaa kama vile thamani , kemikali za
mabara,makampuni na mashirika yanayotoa zabuni za vyakula pamoja na
mifuko ya hifadhi za jamii.
Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
MOENESHO HAYO YATAANZA TASMI TAREHE 17 HADI 21 DESEMBA KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE MAARUFU KAMA SABASABA.
No comments:
Post a Comment