Wafanyakazi wa kituo cha redio 5
Arusha wakikabidhi misaada mbalimbali katika kampeni ya
“USHINDI”inayoendeshwa na kituo hicho,misaada hiyo ilitolewa na wahisani
mbalimbali kwaajili ya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima
Mkoani Arusha,katika Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto ni
Sarah Keiya wakiwakabidhi watoto wa kituo cha kiwohede ndoo ya mafuta
ya kupikia kwaajili ya sikukuya Krismass na mwaka mpya jijini hapa jana
katika hotel ya world Garden
Wafanyakazi
wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo
cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono
jijini Arusha katika tam
Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma
Watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima wakishindana kucheza muziki
Grace Joseph(12)wa kituo cha Kiwohede akionyesha ujuzi wake wa kucheza katika shindano
Mtoto anayeishi katika mazingira magumu akiwa jukwaani akiimba wimbo wa “NISEME”wimbo wa Ya moto band
Mashindano yakiwa yanaendelea
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa mzigoni
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky
Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba moja katika
shindano la kucheza muziki
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky
Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba mbili baada
ya kushinda katika shindano la kucheza muziki
Wafanyakazi wa redio5 wakiwa wanaanda sausage kwaajili ya watoto yatima
Muonekano wa watoto wakiwa katika eneo la kuchezea michezo mbalimbali
Meneja ubunifu wa Redio 5 Bi.Vicky Mwakoyo akiwa na Meneja masoko wa Redio 5Bi.Sarah Keiya
Mtangazaji wa kituo hicho Akiba
Kilango ambaye alikuwa MC wa shughuli hiyo akiwa anaongea na watoto
jukwaani kabla ya mashindano ya kucheza kuanza
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo
Kampuni Tan Communication Media
inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha
imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina
“Kampeni ya USHINDI”linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa
Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho
Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na
tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao
wasijione kutengwa
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky
Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao
ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na
tukifanya hivi watajiskia vizuri
Meneja masoko wa Redio 5 Sarah
Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa
kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio
5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful
company,World garden.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
No comments:
Post a Comment