Wanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mzee Yusuf (kushoto) wakipozi baada ya kufanya mahojiano na wanahabari leo.
Wanamuziki hao wakionyesha mbwebwe zao mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Naseeb
Abdul ‘Diamond Platnumz’ akihojiwa na wanahabari leo katika ofisi za
Global Publishers Ltd tayari kwa Tamasha la Wafalme kesho, Dar Live.
Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akihojiwa na mwanahabari wa Channel Ten, Freddy Mwanjala.
Mzee Yusuf naye akihojiwa na Freddy Mwanjala wa Channel Ten.
Meneja
Mkuu wa Global Publishers Ltd na Dar Live, Abdallah Mrisho (kulia)
akielezea kwa wanahabari jinsi Dar Live walivyojipanga kwa ajili ya
kuwapa burudani safi mashabiki hapo kesho.
Diamond akifurahia jambo na Mzee Yusuf aliyekuwa ‘busy’ na simu yake baada ya mahojiano.
WASANII mahiri nchini Naseeb Abdul
‘Diamond Platnumz’ na Mzee Yusuf wamewaahidi mashabiki wa burudani
hususani wa Jiji la Dar es Salaam kutokosa kesho katika Ukumbi wa Dar
Live kushuhudia shoo ya kibabe inayotambulika kama Tamasha la Wafalme.
Wakiongea na wanahabari katika
Ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ltd zilizopo Mwenge-Bamaga jijini
Dar, wakali hao wamesema wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya shoo hiyo
itakayoacha historia katika pande za Mbagala-Zakhem, jijini Dar.
Naye Meneja wa Dar Live, Abdallah
Mrisho amewataka mashabiki wa burudani kuhudhuria kwa wingi kesho katika
Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live maana kila kitu kiko safi kuanzia
ulinzi na huduma zote muhimu.
Shoo hiyo ya aina yake itaanza asubuhi kwa burudani za watoto
ambapo kundi la sarakasi la Masai Worriors litahakikisha linatoa
burudani ya nguvu kwa watoto wote kwa kuwapa staili mbalimbali za
sarakasi na mazingaombwe.
Pia watoto wataburudika na michezo kibao kama vile kuogelea,
kubembea, kuteleza huku kila mmoja atakayehudhuria kurudi na zawadi
kemkem nyumbani kwao.
Kiingilio cha Tamasha la Wafalme kitakuwa shilingi 10,000 kawaida wakati kwa VIP kiingilio kikiwa shilingi 20,000.
WOTE MNAKARIBISHWA!
No comments:
Post a Comment