Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa Olivier Giroud alihitaji kupewa
kadi nyekundu katika mechi dhidi ya QPR,lakini akathibitisha kuwa
mshambuliaji huyo ameomba msamaha baada ya kisa hicho.
Giroud mwenye miaka 28 alionekana akimpiga kichwa Nedum Onuoha katika kipindi cha pili cha ushindi wa 2-1.Wakati huohuo mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho anasema kuwa beki John Terry anacheza kama wakati alivyoiongoza the blues kushinda ligi ya Uingereza miaka kumi iliopita.
Ana motisha chungu nzima.
Terry alifunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham na kuifanya timu hiyo kusalia kileleni mwa ligi hiyo.
Kwengineko mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa ametosheka na uongozi unaotolewa na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney ambaye alicheza katika safu ya kati na kuisadia timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford.
Rooney alifunga mabao mawili na kutoa usaidia wa bao la tatu kwa Robin Van Persie.
Nayo Manchester City ilifunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza dhidi ya West Bromwich licha ya barafu iliokuwa ikianguka katika uwanja huo na kusalia nyuma ya Chelsea kwa alama tatu.
Fernando aliifungia City bao la kwanza,baada ya Ben Foster kutoa kross nzuri kutoka kwa Jesus Navas.
West Bromwich walifunga bao la kufutia machozi wakati wa kipindi cha pili.
Hivi ndivyo ilivyokuwa:
Chelsea 2 - 0 West Ham
Burnley 0 - 1 Liverpool
Crystal Palace 1 - 3 Southampton
Everton 0 - 1 Stoke
Leicester 1 - 2 Tottenham
Man Utd 3 - 1 Newcastle
Sunderland 1 - 3 Hull
Swansea 1 - 0 Aston Villa
West Brom 1 - 3 Man City
Arsenal 2-1 QPR
No comments:
Post a Comment