MIILI YA WATU 14 WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MELI YA CONGO YAIBUKA KIGOMA JUMLA ya maiti 14 zimezikwa baada ya makubaliano baina ya serekali ya Tanzania na serekali ya Demokrasia ya Congo(DRC)ambapo katika mazishi hayo serekali ya Congo iliwakilishwa na Balozi wa Congo kutoka ubalozi mdogo wa DRC Mkoani Kigoma.
Akizungumza muda mfupi baada ya mazishi ya
raia hao Balozi mdogo wa DRC nchini kutoka Ubaozi mdogo Mkoani hapa,Mh.
Riki Moleme alisema. Mh. Maleme alisema kuwa amefarijika sana kwa namna
serekali ya Tanzania ilivyochukulia kwa umuhimu mkubwa swala la maafa
hayo ya Raia wa Congo na namna ilivyojitoa kushughulikia mazishi ya
miili hiyo Naye Mhifadhi wa mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mahale,Herman
Batiho alisema alianza kuona miili ya watu majira ya jioni ya Desemba 20
Mwaka huu na ndipo walipoamua kutoa taarifa katika mamlaka mbalimbali
ambapo waliwasiliana na uongozi wa kijiji cha kalilani ambapo uongozi wa
kijiji kwa kushirikiana na wanachi walianza kazi ya uopoji wa miili.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kalilani,Songoro Saidi alisema kuwa waliona
moja ya mili wa maiti hizo asubuhi ya Desemba 21 ukiwa umeibuka juu,pia
walipata kuwepo kwa miili mingine ikiibuka na kuelea ndani ya Hifadhi ya
Mahale na ndipo waliposhirikiana kuipoa miili hiyo na hadi kufanikisha
mchakato wa mazishi.
Desemba 12 mwaka huu ya watu 128 walifariki dunia
na wengine 250 waliokolewa kufuatia meli waliyokuwa wakisafiria kutoka
Mobaa kuelekea Kalemii kuzama katika mwambao mwa ziwa Tanganyika katika
Mkoa wa Kalemii nchini DRC Askari wa jeshi la ulinzi wa
Tanzania(JWTZ)wakiwaongoza viongozi wa serekali ya Tanzania na Congo na
viongozi wa kijiji cha Kalikani pamoja na wananchi katika mazishi ya
raia 14 wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo(DRC) waliofariki katika
ajali ya meli Desemba 12 mwaka huu katika Mkoa wa Kalemi na miili yao
kuibuka katika Hifadhi ya Mhale. Picha na Editha Karlo wa Globu ya
Jamii, Kigoma
No comments:
Post a Comment