AITWAYE
JOHN EMANUEL (36) MKAZI WWATU TISA [09] KATI YAO WANAUME SABA [07] NA
WANAWAKE WAWILI [02] WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALIOKUWA
WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.203 ARZ AINA YA TOYOTA COASTER
LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
A MLOWO-MBOZI LIKIWA LINATOKEA
MBEYA KWENDA TUNDUMA WAKATI AKIJARIBU KULIPITA GARI T.789 AZL/T.123 AXV
AINA YA TATA TRUCK ENEO AMBALO KUNA MLIMA NA MBELE YAKE KUNA KONA
LILITOKEA GARI T.903 CVF AINA YA TATA BASI HIVYO DEREVA WA COASTER
KULAZIMIKA KUINGIA MBELE YA LORI ALILOKUWA ANALIPITA NA KUGONGWA UBAVUNI
UPANDE WA KUSHOTO PIA KUGONGWA UPANDE WA KULIA NA BASI AINA YA TATA
TAJWA HAPO JUU.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
21.12.2014 MAJIRA YA SAA 14:10 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHENGULA,
KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, BARABARA KUU
YA MBEYA/TUNDUMA. MAREHEMU WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA NI WANNE AMBAO NI
1. THOMAS SIMFUKWE (35) 2. EXAVERY MUMBISA (34) 3. AMINA MAIKO (30) 4.
NEEMA ALMASI 5. HEBELI MKILIMI 6. ROSE HEZRON HALELE NA 7. ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA MOJA JANUARI.
HATA HIVYO MIILI YA MAREHEMU
WATATU BADO KUTAMBULIWA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU KUMI NA MOJA [11]
WALIJERUHIWA AMBAO MAJERUHI SITA [06] WANAUME, WANNE [04] WANAWAKE,
WAWILI WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA AMBAO NI DEREVA AITWAYE
JOHN EMMANUEL MZUMBA (36) MKAZI WA MLOWO NA KONDAKTA AITWAYE CHRISTIAN
MTENDE (31) MKAZI WA MLOWO NA WENGINE SABA WALIPELEKWA KATIKA HOSPITALI
YA SERIKALI WILAYA YA MBOZI NA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KWA MATIBABU.
CHANZO CHA AJALI NI UZEMBE WA DEREVA WA TOYOTA COASTER KUTAKA KUYAPITA MAGARI YALIYOKUWA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
DEREVA WA LORI ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA HAMAD AHMAD @ MASAWE (30) MKAZI WA DSM AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO
BAADA YA GARI ALILOKUWA AKIENDESHA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.769 ARX
AINA YA SCANIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA ENEO LA SENJELE WILAYA YA MBOZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
21.12.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SENJELE,
KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, BARABARA KUU YA
MBEYA/TUNDUMA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHUIWA HASPITALI YA SERIKALI YA WILAYA YA MBOZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 08
ALIYETAMBULIKA KWA JINA SHIMBI MWANDU MKAZI WA KIJIJI CHA MKUNYWA
ALIKUTWA AMEKUFA MAJI KATIKA MFEREJI UNAOPELEKA MAJI KATIKA MASHAMBA YA
MPUNGA WILAYANI MBARALI
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KATIKA
MFEREJI HUO MNAMO TAREHE 21.12.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MLONGA, KIJIJI CHA MKUNYWA, KATA YA MADIBIRA,
TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA KUWA
MAREHEMU ALIKUNYWA MAJI MENGI NA KUKOSA HEWA AKIWA NDANI YA MAJI YA
MFEREJI HUO HALI ILIYOPELEKEA KIFO CHAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA
MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA. AIDHA
ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA, KUFUKIA MASHIMO NA MITARO KWANI
NI HATARI KWA WATOTO.
R Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment