

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ambao waliitika wito wa kumsikiliza wakati wa kulihutubia Taifa kupitia Wazee kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.( Picha na Adam Mzee

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kwa Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ( Picha na Adam Mzee)
Baadhi ya Wanasiasa wakongwe waliohudhuria.
Kila wilaya ya mkoa wa Dar es salaam iliandaliwa sehemu maalum ya kukaa.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Taifa kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es
Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alizungumzia uchaguzi na
kutaka polisi kufanya kazi yao katika kuhakikisha uchaguzi ujao uchaguzi
hauvurugwi na pia alifafanua mambo mbali mbali yaliyokuwa
yakizungumziwa kuhusu akaunti ya ESCROW na kumwajibisha Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Ukumbi
wa Diamond Jubilee ukiwa umefurika Wazee waliokuja kumsikiliza
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Ukumbi ulifurika kila kona.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa ufafanuzi wa masula
kadhaa yaliyoleta mkanganyiko kwenye sakata la Escrow Akaunti.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akipanga
makaratasi yenye hotuba yake wakati wa kuhutubia Wazee wa mkoa wa Dar es
Salaam.
Wananchi
wakishangilia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuhitimisha hotuba yake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es
Salaam.

No comments:
Post a Comment