Na:
Zaidi ya nyumba hamsini na moja zinazokadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya miambili katika manispaa ya Singida zimebomolewa na mapaa yake kuezuliwa na mvua kubwa iliyonyesha ya mawe ikiwa na upepo mkali iliyo dumu kwa dakika ishirini.
Mvua hiyo ambayo ilianza kunyesha majira ya saa kumina mbili jioni
siku ya tarehe ishirini na tatu imesababisha hasara kubwa kwa wakazi wa
manispaa ya Singida, jitihada za kumpata mkuu wa wilaya ya Singida Bi
Queen Mlozi ili kuelezea tukio hili zimepatikana na kueleza kuwa mpaka
sasa nyumba hamsini na moja zimeharibiwa ikiwemo nyumba za watu binafsi
na madarasa ya msikiti na kusema kuwa serekali imejipanga kuwasaidia
watu walio athirika.
Akieleze diwani wa kata ya mitunduruni Bwana Pantaleo Sorongai
amesema mvua iliyonyesha imeleta madhara makubwa na ameomba serekali
kutoa msaada wa mahema na chakula kwa wakazi ambao wameathirika kwani
hawana sehemu za kujisitiri.
Kwa upande wao wakazi wa manispaa ya Singida wamesema mvua iliyo
nyesha haija wahi kutokea pamoja na kunyesha muda mfupi imeleta madhara
makubwa na wamelalamikia manispaa ya Singida kwa kutokutengeneza vizuri
miundombinu ya maji na kusababisha nyumba nyingi kubomoka.
No comments:
Post a Comment