Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu
Nchemba anatarajiwa kuongoza Tamasha Maalumu la ‘Upendo wa Mama’
linalotarajiwa kufanyika katika Kanisa la Rutheran Mabibo Extenal jijini
Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji wengi kutoka ndani na nje ya
Tanzania.
Akizungumzia tamasha hilo leo
jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya Upendo kwa Mama Foundation
yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia Carlos Mkundi alisema
Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha hilo maalumu ambalo
pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua mchango mkubwa wa mama
kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima.
Injinia Mkundi alisema tamasha
hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015 chini ya uratibu wa Taasisi ya
Upendo kwa Mama Faundation, litashirikisha waimbaji wa injili akiwemo
Faraja Ntaboba kutoka Congo, Stella Joel, Ado Novemba, Jane Misso, Edson
Mwasabwite wote kutoka jijini Dar es Salaam. Na Rose Molel, Helen
Kigazi wote kutoka mkoani Arusha.
Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji
wa muziki wa injili ambaye naye atatumbuiza katika tamasha hilo,
aliwataja waimbaji wengine ambao watashiriki katika tamasha ni pamoja na
Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini
Njole, Messi Chengula na waimbaji wengine wengi.
“…Washiriki kila mmoja anaweza
kuja na mamayake anayempenda pamoja na zawadi yake maalum, ambayo
atamkabidhi wakati itakapotangazwa…kutakuwa na waimbaji wa muziki wa
injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta mvuto zaidi tunawaomba
wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango wa mama na kuonesha
upendo kwa mama zao,” alisema Injinia Mkundi.
Akifafanua zaidi alisema Tamasha
la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na litaanza majira ya saa saba
mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni litakapofungwa. Alisema siku
hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi maalumu ambayo kila mmoja
atamkabidhi mamayake anayempenda katika familia zao.
Rais wa Taasisi ya Upendo kwa Mama
Faundation, Injinia Caros aliongeza kuwa lengo lingine ni pamoja na
kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha upendo juu ya kazi kubwa
wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa ujumla.
Alisema baada ya uzinduzi wa
tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa matamasha mengine makubwa na
kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa pamoja na mengine
katika mikoa mbalimbali. Aidha aliongeza tamasha kama hilo pia
lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.
No comments:
Post a Comment