Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara(MB)
akikagua timu za Vijana waliochini ya miaka 15 kutoka Kinondoni na
Dodoma ambazo zilishiriki hatua ya fainali katika mashindano ya Copa
Coca Cola mwishoni mwa wikiendi katika uwanja wa Krume jijini Dar es
Salaam. Ambapa katika fainali hizo kwa upande wanaume toimu kutoka
Dodoma iliibuka bingwa wa mashindano hayo kwa kuichapa Kinondoni jumla
ya magoli 4 -0, wakati kwa upande wa wanawake Kinondoni ilinyakua
ubingwa kuifunga Ilala kwa mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni
kumaliza kwa sare ya mbili mbili.
Mchezaji
wa timu ya mpira wa miguu wanawake kutoka Kinondoni akifunga penati
wakati wa fainali za Copa Coca Cola 2014 katika mchezo uliochezwa kwenye
uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mapema wikiendi hii, Kinondoni
ilinyakua ubingwa kwa kuifunga Ilala mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya
dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili mbili.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(MB) (wa tatu kutoka kushoto) akifurahia mara baada ya kukabidhi zawadi
ya mchezaji bora wa kike katika mashindano ya Copa Coca Cola kwa
Golikipa wa timu ya Kinondoni Zubeda Mohamed (15). Wakwanza kutoka
kushoto ni Meneja Masoko wa Coca Cola Bw. Godfrey Njowoka, Rais wa TFF
Jamal Malinzi na nyuma ya waziri anayecheka ni Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Michezo Leonard Thadeo.
Mashabiki wakifuatilia fainali za Copa Coca Cola 2014
No comments:
Post a Comment