Wamiliki
wa Internet Cafe jijini hapa wametakiwa kuwa makini na wateja wao
hususani watoto wadogo ambao hutumia huduma hizo kinyume kwa kuangalia
Picha za ngono ambapo huchangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili
ya mtoto wa Kitanzania.
Wito huo umetolewa leo jijini hapa na Kamanda wa polisi wa jiji
hili la Arusha liberatus Sabas alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari ofisini kwake ambapo alisema amekuwa akisikitishwa na watoto wa
karne hii ya sasa kwa kupenda kuangalia Picha hizo ambazo Haziwezi
kuwajenga Kimaadili.
Alisema hivi sasa watoto wengi wamekuwa wakijidanganya asa kwa
kupenda kufanya vitu ambavyo havina manufaa kwa maisha yao ya Baadae
kitendo kitakachowafanya wje kuwa na muelekeo mbaya katika maisha yao ya
baadae.
“Sidhani kama watoto wetu watakuja kuwa na masiha mazuri hapao
baadae kwani abadala ya kujitahidi kuongeza bidii katika masopmo ambapo
ndio mkombozi wa maisha yao Jamii kwa ujumla tuwakomboeni watoto
wetu”Alisema kwa masikitiko makubwa.
Pia aliwaomba wazazi kuwa makini na watoto wao huku wakijitaidi
wanakuwa katika hali inayostaili kimaadili ya mtoto wa kitanzani badala
ya kuwaacha waige utamaduni wa kizungu ambapo hautakuwa na faida yeyote
katika maisha yao ya Baadae.
“wapo baadhi ya wazazi hhupenda watotot wao kuiga tamaduni za
kizungiu kuanzia mavazi wanayovaa wataoto hao mpaka katika saula zima la
kimaadili,Sisis ni Watanzania jamani achaeni mitindo ya kuiga
tunawafundisha nini watoto wetu jamani?”alihoji kwa jazba Matei.
Akiendelea kuzungumzia suala hilo kamanda Matei alisema endapo
wazazi kwa kushirikiana na jamii kwa ujumla kukubali watoto wao kukanywa
na kila pindi wanapokutwa waiaangalia picha hizo basi kwa namna moja
ama nyingine wataweza kupunguza tatizo ingawa si wazazi wote wanaopenda
watoto wao kurekebishwa na watu wengine pindi wanapokosea.
No comments:
Post a Comment