Rais Dr Jakaya Kikwete
amemuachisha kazi waziri wa Arhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka
kutokana na tuhuma za kupata mgao wa Fedha za Akaunti ya Escrow kiasi
cha bilioni Moja na Milioni Mia Sita ambazo alidai amepewa mchango kwa
ajili ya shule, Rais Jakaya amesema Tumeamua mwenzetu huyu atupishe ili
tuchague mtu mwingine wa kuhudumu katika wizara hiyo kutokana na maswali
magumu.
Akiwa kama Mtumishi wa serikali
ambaye anatakiwa kufuata maadili ya Utumishi wa umma aliamua kupokea
kiasi kikubwa cha fedha huku akijua kimaadili kama mtumishi wa serikali
haitakiwi, Rais Dr. Jakaya Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na
taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wiazara hiyo
Eliackhim Maswi amesema ameagiza uchunguzi ufanyika na katika muda wa
siku mbili au tatu hivi atapewa taarifa ya uchunguzi huo na kuchukua
hatua stahiki.
Na Kwa upande wa Majaji wa
Mahakama Kuu waliotuhumiwa Rais Dr. Jakaya Kikwete amesema anamwachia
Jaji Mkuu Mh. Jaji Mohammed Chande Othman ili achukue hatua za kimaadili
kutokana na taratibu za kimahamama na mara baada ya kujiridhisha
atapewa taarifa na Jaji mkuu na kuchukua hatua.
No comments:
Post a Comment