Wapiganaji
wa kundi la Islamic State wamesema kuwa waliidungua ndege ya jeshi la
muungano ,lakini Marekani inasema kuwa ushahidi uliopo unaonyesha kuwa
hilo si kweli.
Jordan ni miongoni mwa mataifa manne ya kiarabu
yaliopo katika muungano wa majeshi yanayoungwa mkono na Marekani ambayo
yameanzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa IS.
Ndege hiyo
aina ya F-16 ni ndege ya kwanza ya jeshi hilo la muungano kupotea katika
maeneo yanayodhibitiwa na IS tangu mashambulizi yaanze mnamo mwezi
Septemba.
Picha za IS zinamuonyesha rubani wa ndege hiyo akikamatwa.
Wamemtaja rubani huyo kuwa Moaz Youssef al-Kasasbeh.
Wakati
huohuo Jordan imesema kuwa hasara iliyopata ya kupoteza ndege yake moja
ya kivita, katika anga linalodhibitiwa na waasi wa Islamic State,
haitayumbisha majeshi yake kuendelea kukabiliana na matendo ya kigaidi.
No comments:
Post a Comment