Mchuungaji Mpeli akiwashukuru wadau |
Watoto yatima wakifurahia msaada huo |
wageni mbali mbali waliofika katika hafla hiyo |
Sarah Mungai na Mumewe Geofrey wakitoa taarifa yao fupi |
Mmoja wa watoto yatima akishukuru |
Geofrey na mkewe wakiwaongoza yatima kupata chakula |
Mtoto aliyetupwa |
Dr Gabone akishiriki chakula |
Mungai akimlisha chakula yatima |
……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
MKANDARASI Geofrey Mungai ametoamsaada wa nguo za sikukuu na
chakula vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 wa kituo cha
watoto yatima cha Daily Bread Life Tanzania (DBL) kwa ajili ya
kusherekea sikukuu ya krismass na mwaka mpya.
Mungai alitoa msaada huo jana kwa uongozi wa kituo hicho pamoja na kuwaandalia chakula cha pamoja watoto zaidi 39 na wananchi mbali mbali wa mji wa Iringa kama njia ya kuwahamasisha kusaidia yatima .
Akizungumza kwa niaba ya familia ya Mungai mke wa mkandarasi huyo Sarah Mungai alisema kuwa imekuwa ni kawaida yake kwa kila mwaka katika msimu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kufika katika kituo hicho na kuwapa msaada watoto hao ili nao kuungana na watoto wenye wazazi wao kufurahia sikukuu hizo.
Hata hivyo alisema kuwa jamii ya mkoa wa Iringa na watanzania kwa ujumla wanapaswa kubadilika kwa kuelekeza michango yao kwa watoto yatima ambao baada ya kupoteza wazazi wao faraja ya pekee wanaisubiri kutoka kwa jamii inayowazunguka.
Aidha alisema kuwa yeye kama mmoja kati ya wananchi wa Iringa wenye
mapenzi mema na watoto yatima hivyo kuwaomba wananchi wengine kuweka
mpango wa kuendelea kutembelea vituo vya yatima kila mwaka kwa ajili ya kuwasaidia misaada mbali mbali.
kuwa upo uwezekano mkubwa wa watoto hao yatima kuendelea kusaidia iwapo watanzania na wadau mbali mbali kuwekeza kwa watoto hao.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbi mbali ya kumpongeza Mungai kwa kuendelea kusaidia watoto hao bado wadau mbali mbali wameendelea kujitolea kusaidia kituo hicho .
“watoto hao wanalilewa vema na wapo ambao wanasoma shule mbali mbali na vyuo vikuu baada ya kusaidiwa na wadau” Alisema kuwa kituo hicho kinafanya kazi chini ya shirika lisilo la kiserikali ya Daily Bread Life Tanzania lililosajiliwa kwa usajili 12903 chini ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi pia kituo kimesajiliwa na ustawi wa jamii kwa kupewa usajili wa makao ya watoto namba 00049995.
Hata hivyo alisema kuwa kituo kilianza kupokea watoto 14 mwaka 2004
na sasa kuna watoto 37 waliopo kituoni hapo na kuwa toka kituo kianzishwe jumla ya watoto 51 wamelelewa hapo Alisema kutokana na misaada wa wadau mbali mbali kituo kimeendelea kupata mafanikio makubwa kama kuwa na shamba ,basi moja ,mradi wa cherehani pia tayari shule ya sekondari ya DBL imejengwa na imeanza kupokea wanafunzi toka mwaka huu shule iliyopo umbali wa kilomita 6 kutoka mjini Iringa kwa lengo kuwawezesha watoto na wengine watyakaofaulu na kukosa nafasi kupata elimu ya sekondari.
Pia alisema changamoto kubwa katika uendeshaji wa kituo hicho ni michango mingi katika shule za msingi ambako watoto hao wanasoma ,kukosa ruzuku toka serikalini na changamoto nyingine nyingi.
Mchungaji Mpeli aliwaomba watanzania na wadau mbali mbali pale walipo iwapo wanahitaji kusaidia kituo hicho kutuma michango yao kupitia
Akaunti namba Benk ya Exim ni 5435526007 Daily Bread Life Childreans home ,ama kwa njia ya Na M-PESA 0754362536
No comments:
Post a Comment