MENEJA
wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa nahodha wake Mikael
Arteta atachelewa kidogo kupona majeruhi yanayomsumbua lakini kiungo
Aaron Ramsey anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo dhidi ya Southampton
wakati wa mwaka mpya.
Arteta alipata majeruhi mwezi uliopita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund.
Wenger
amesema nahodha wake huyo anaendelea vyema lakini atachelewa kidogo
kuliko ilivyotegemewa lakini Ramsey anaweza kurejea katika mchezo dhidi
ya Southampton.
Ramsey alikuwa akirejea katika kiwango chake cha
msimu uliopita akiwa amefunga mabao matatu katika mechi mbili kabla ya
kutolewa wakati wa mapumziko katika mchezo dhidi ya Galatasaray mapema
mwezi huu.
Wenger pia amebainisha kuwa Laurent Koscielny naye
anakaribia kurejea katika kikosi cha kwanza na anaweza kuwepo katika
kikosi chake kitakachopambana na West Ham United huko Upton Park.
No comments:
Post a Comment