CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Desemba 14, kimewaliza Viongozi
wa Chama cha CCM Mvomero akiwemo Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala,
ambapo kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wameangukia Pua, kwa Vijiji
vyao kuchukuliwa na Chadema.
Mbali ya Waziri Makala, wengine waliolizwa ni pamoja na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Jonas Van Zealand,
Mwenyekiti wa Wilaya wa CCM, Abdalah Mtiga, Katibu Mwenezi wa CCM,
Yusufu Kingu, Mwenyekiti wa Vijana (UVCCM), Pascal Boge.
Akizungumza na Tanzania Daima, Diwani wa Chadema Kata ya Mtibwa,
Luka Mwakambaya, alisema, waliolizwa si Waziri Makala na Wenzake tu
wilayani, bali Serikali yote ya Mji Mdogo wa Madizini, Viti vyote
vimechukuliwa na Chadema, na Viongozi wa CCM wako mafichoni.
“Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mtibwa, Aloyce Msigwa, Mwenyekiti
UVCCM, Ponsian John, wamepigwa vijijini mwao, Khalifa Ahmed (Chadema),
akinyakua Uenyekiti wa Kijiji cha Mji Mdogo wa Madizini, uliosababisha
Viongozi wote wa CCM kujificha”.alisema Mwakambaya.
Licha ya Wananchi kushangilia Kuchaguliwa Mwenyekiti wa Kijiji
cha Lungo, Sifuni Mzava (CHADEMA), aliyekuwa TLP; Watu wa Mji Mdogo
Madizini-Mtibwa na Turiani wa Vyama vya CCM, Chadema, Chama cha Wananchi
(CUF) na Vyama vingine, walipohijiwa walisema,
“Kama Taifa linavyomuenzi Mwasisi, Mwalimu Julus Nyerere, bila
Kujali Itikadi zetu, tumepiga Kura kumuenzi Diwani wetu, Marehemu
Tusekile Mwakyoma (Chadema), aliyefariki kwa kuchomwa Kisu, kutokana na
kukataa wananchi tusinyanyaswe na Mwekezaji wa Mtibwa”.
Awali ushindi wa Chadema, umeelezwa umetokana na Ushirikiano wa
Watu, Viongozi wa Chadema akiwemo, aliyekuwa Mgombea wa Ubunge wa
Mvomero, Matokeo Wordern, ambaye wanachadema wanadai ushindi wake
ulichakachuliwa, ndio walikuwa chachu ya Ushindi huo.
No comments:
Post a Comment