Mke
wa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Simone Gbagbo
amefikishwa mahakamani kutokana na mashtaka ya kuhusika kwenye ghasia za
baada ya uchaguzi ambapo zaidi ya watu 300 waliuwa.
Bi Gbagbo na
watu wengine 82 akiwemo waziri mkuu wa zamani wameshtakiwa kwa kuhujumu
usalama wa nchi, ukabila na kwa kubuni makundi ya uhalifu.
Rais wa
zamani Laurent Gbagbo ambaye alikataa kukubali kushindwa kwenye
uchaguzi mkuu miaka minne iliyopita anasubiri kesi yake kwenye mahakama
ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kutokana na mashtaka ya uhalifu
dhidi ya ubinadamu.
Zaidi ya watu 3000 waliuawa katika ghasia hizo baada ya rais huyo wa zamani kukataa kushindwa katika kura ya awamu ya pili.
Bi
Gbagbo ambaye alikuwa anazuiliwa katika kifungo cha nyumbani kwa miaka
mitatu ameshtakiwa kwa jaribio la kuhujumu usalama wa taifa hilo.
Aliyekuwa waziri mkuu Gilbert Ake N'Gbo na kiongozi wa chama cha FPI Affi N'Guessan pia wamefunguliwa mashtaka na bi Gbagbo.
No comments:
Post a Comment