TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 25, 2014

BAADA YA MISS TANZANIA KUFUNGIWA,(BASATA) WASHAULIWA KUTOA NAFASI KWA WABUNIFU WANAOJITOKEZA ILI KUONYESHA MABADILIKO NA MBINU MPYA, MIFUMO MIPYA KWA LENGO LA KUENDANA NA MABADILIKO NCHI.








Leo December 25 kuna taarifa kwamba Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali za ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.

Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.

“Baada ya kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea arejee kwa nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa…“– Mngereza.





Shindano hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo, pamoja na kuandamwa kwa washiriki wengi baada ya kuingia kwenye Shindano hilo matokeo yamekuwa ni baada wakati wanapoutumia umaarufu wa mafunzo yao Vibaya ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi yasiyostahili wakati wa kufikisha taarifa na UJumbe kwa jamii, kitendo kinachosababisha wazazi wengi kupiga Kelele ikiwa ni pamoja na kuwakataza vijana wao kushiriki kwenye shindano hilo kwa kile kinachodaiwa kufundishwa maadili mabovu yanayoleta aibu kwa Taifa.
 
Kitendo cha Kulifungia Shindano la Miss Tanzania sasa kinakuwa ni cha Pili kuyafungia Mashindano ya Urembo yaliyotangulia ikiwemo la Miss Utalii ambalo pia Limefungiwa kwa uendeshwaji Mbovu ikiwa ni pamoja na washiriki wengi kulalamikia kufanyia vitendo vya uzalilishwaji ikiwemo kuombwa Rushwa ya Ngono na Waandaji huku rushwa ikitawala na kusababisha Washindi halali kunyimwa haki zao.
 
Lakini hata hivyo Serikali kupitia Mamlaka husika(BASATA)wanatakiwa kutotumia Madaraka waliyonayo Vibaya kwa kujaribu Kuyakumbatia Mashindano Hayo huku Wabunifu wengine wa Mashindano ya Urembo Wanapojitokezwa kujaribu kutaka kuonyesha Mifumo Mipya ya Uendeshwaji wa Mashindano unaokidhi haja ya Watanzania kwa kuonyesha aina Mpya za Mavazi, pamoja na Mifumo mipya ya Uendeshwaji inyoendana na Demokrasia ya Watu kunyimwa Vibali kutokana na Kukumbati na kuwa na Ushabiki ndani ya Mashindano hayo ambayo hata hivyo(BASATA) wameyafungia kutokana na shinikizo kutoka kwa wananchi ambao wamechoshwa na Vitendo vuilivyokuwa wakifanyiwa na kuendelea kila Mwaka katika Mashindano hayo.
 
kuna haja sasa ya (BASATA) kuangalia Upya Baadhi ya Wabunifu wanaojitpokeza kuwa na Mashindano yanayoendana na Ushirikishwaji wa Wasichana wetu katika Mashindano ya Urembo, ili waweze kuruhusiwa kuendesha Mashindano hayo bila kuingiliana na Mashindano yaliyotangulia, maana kuwanyima nafasi ya kufikisha Ubunifu huo kwa hao wabunifu wapya ni kuwanyima haki yao kimsingi ya kutumia Fulsa ya kujitambua na kunyimwa haki kitendo ambacho ni ukiukwaji wa Haki za Binadamu kutumia Uhuru walionao kwa Taifa lao.

No comments:

Post a Comment