Mashindano
ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake)
yanazinduliwa rasmi Januari Mosi mwakani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza kwa mechi kati ya wenyeji Mwanza na Mara.
Mechi hiyo itakayoonyeshwa moja
kwa moja na televisheni ya Azam itachezwa kuanzia saa 10 jioni.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin yatachezwa kwa
mtindo wa nyumbani na ugenini katika hatua ya kwanza
Januari 10 mwakani ndipo
zitachezwa mechi kwa mikoa yote ambapo Geita itakuwa mwenyeji wa Kagera
(Uwanja wa Geita), Tabora vs Kigoma (Ali Hassan Mwinyi), Simiyu vs
Shinyanga (Uwanja wa Simiyu), Arusha vs Manyara (Sheikh Kaluta Amri
Abeid), na Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja wa Ushirika).
Mechi nyingine ni Lindi
itaikaribisha Mtwara kwenye Uwanja wa Ilulu, Ruvuma vs Njombe (Uwanja wa
Majimaji), Mbeya vs Iringa (Uwanja wa Sokoine), Katavi vs Rukwa (Uwanja
wa Katavi), Dodoma vs Singida (Uwanja wa Jamhuri) na Pwani itakuwa
mwenyeji wa Morogoro katika Uwanja wa Mabatini.
Timu hizo zitarudiana Januari 13
mwakani, ambapo baada ya matokeo ya nyumbani na ugenini timu iliyoshinda
ndiyo itakayoingia hatua inayofuata ambayo pia itashirikisha mikoa ya
kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke.
Hatua hiyo, mechi zake za kwanza zitachezwa Januari 17 mwakani wakati zile za marudiano zitafanyika Januari 21 mwakani.
Baada ya hapo, hatua itakayofuata
ni robo fainali, nusu fainali na fainali ambayo ndiyo itakayotoa bingwa
wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini.
Mdhamini atatoa jezi kwa timu zote zinazoshiriki kabla ya kuanza mashindano hayo.
SDL KUTIMUA VUMBI KRISMASI
Michuano ya Ligi Daraja la Pili
(SDL) inayochezwa katika makundi manne tofauti inaingia raundi ya nne
kesho (Desemba 25 mwaka huu) kwa mechi ya kundi C kati ya Kiluvya United
na Abajalo itakayochezwa Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani
Pwani.
Mechi nyingine ya kundi hilo kati
ya Mshikamano FC na Transit Camp yenyewe itachezwa keshokutwa (Desemba
26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es
Salaam.
Kundi A litakuwa na mechi Jumamosi
(Desemba 27 mwaka huu) ambayo itazikutanisha timu za Ujenzi Rukwa na
Mji Mkuu (CDA) kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Desemba
28 mwaka huu ni kati ya Mvuvumwa FC na Milambo SC kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika mjini Kigoma.
Jumamosi (Desemba 27 mwaka huu)
kundi B litakuwa na mechi kati ya Arusha FC na Pamba (Uwanja wa Sheikh
Kaluta Amri Abeid jijini Arusha), na Mbao FC vs JKT Rwamkoma (Uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza).
Kundi D siku ya Jumamosi hekaheka
itakuwa kati ya Mkamba Rangers na Volcano (Uwanja CCM Mkamba), Njombe
Mji vs Wenda FC (Uwanja wa Amani, Njombe) na Town Small Boys vs Magereza
FC (Uwanja wa Majimaji, Songea).
Ratiba ya michuano ya Taifa Cup Wanawake pamoja na msimamo wa SDL vimeambatanishwa (attached).
No comments:
Post a Comment