Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge
wa Ubungo, John Mnyika, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Taasisi
ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania kwa ajili ya kuzindua
Taasisi hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2014.
Picha zote na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake
wakati akizindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam,
leo Desemba 22, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto)
akikata utepe kuzindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria
kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika
jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Waziri wa
Katiba na Sheria, Angela Kairuki, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuweka
Jiwe la Msingi katika Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo hayo
uliofanyika leo Desemba 22, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa
kumbukumbu katika eneo la viwanja vya Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya
Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, baada ya kuzindua rasmi majengo hayo
yaliyopo eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam leo Desemba 22, 2014.
No comments:
Post a Comment