Waziri
mpya wa usalama nchini Kenya, Joseph Nkaissery ameapishwa rasmi na
kuanza kutekeleza wajibu wake kama waziri akikutoa onyo kali kwa maafisa
wa usalama kwamba ni lazima wawajibike la sivyo watimuliwe.
Jenerali huyo mstaafu anasema raia wa Kenya wana haki ya kupata usalama bora zaidi kutoka kwa maafisa wa polisi.
Nkaissery anamrithi Joseph Ole Lenku aliyetimuliwa kazini na rais Uhuru Kenyatta mwezi uliopita. Emmanuel Igunza anaarifu.
Katika
hotuba yake ya kwanza punde tu baada ya kuapishwa, Nkaissery amesema
anafahamu kuhusu mtazamamo wa umma wa kutokuwa na imani na idara ya
polisi nchini.
Lakini amesema anataka kukabiliana na hili kwa dharura kwa kuwahimiza maafisa wote kuwawajibikia wananchi.
Vilevile
ameitetea sheria mpya ya usalama iliyoidhinishwa hivi maajuzi nchini
ambayo imezusha mjadala mkali. Nkaissery amesema anaamini kwamba sheria
hiyo ya kukabiliana na ugaidi ambayo upinzani unaiona kuwa kali
inayokiuka uhuru wa wananchi itasaidia zaidi katika kukabiliana na
tishio la kundi la wanamgambo wa kiislamu kutoka Somalia, Al Shabaab.
Rais
Uhuru Kenyatta amemteua Nkaissery baada ya msururu wa mauaji
yaliotekelezwa huko kaskazini mashariki mwa Kenya ambayo kundi hilo la
Alshabaab linatuhumiwa kutekeleza. Kundi hilo limetekeleza mashambulio
kadhaa ya kigaidi nchini.
No comments:
Post a Comment