Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (katikati) akiongozana na
Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam
(DAWASCO) , Meja General (mstaafu), Samuel Kitundu (kushoto) na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Cyprian Luhemeja , wakati Waziri huyo
alipoitembelea Dawasco leo na na kisha kutangaza watumishi tisa ambao
ameiagiza bodi kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia
tuhuma mbalimbali. Mhandisi Lwenge alitembelea leo.
WATUMISHI AMBAO WAZIRI AMEAGIZA BODI IWASIMAMISHE KAZI NI:-
Meneja
Rasilimali Watu, Mvano Mandawa, Meneja Ufuatiliaji na Tathmini, Reinary
Kapera, Teresia Mlengu, Emmanuel Guluba, Peter Chacha, Fred Mapunda,
Reginald Kessy, Jumanne Ngelela na Bernard Nkenda.
Aidha Waziri Lwenge aliagiza pia kuchunguzwa kwa CEO wa zamani Jackson Midala.
Miongoni
mwa tuhuma zao ni pamoja na kufanya maunganisho ya maji yasiyofuata
utaratibu kwa kampuni ya STRABAG inayotekeleza mradi wa mabasi yaendayo
kasi na kusababisha kulikosesha shirika mapato yenye thamani ya sh
Bilioni 2.8 (2,887,577,134/=).
Mameneja wa Dawasco wakiwa katika mkutano huo.Baadhi yao walisimamisha kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazo wakabili.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (kulia) akizungumza na bodi
pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es Salaam
(DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika hilo
Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi tisa.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge (aliyesimama) akizungumza na
bodi pamoja na menejimenti ya Shirika la Maji taka na Maji safi Dar es
Salaam (DAWASCO) wakati Waziri huyo alipotembelea makao makuu ya shirika
hilo Dar es Salaam jana na kuiagiza bodi kusimamisha kazi watumishi
tisa.
No comments:
Post a Comment