Mwenyekiti
wa wa chama cha wamiliki wa malori Tanzania (TATOA), Angelina Ngalula
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na
ujenzi wa madarasa 12 katika manispaa ya Temeke.
Sehemu ya Bodi ya TATOA na watendaji wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza na bodi ya TATOA jijini Dar es Salaam leo.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
CHAMA
cha Wamiliki wa Malori nchini (TATOA) kinatarajia kujenga madarasa 12
katika shule msingi maji matitu ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Rais
Dk.John Pombe Magufuli ya kuhakikisha shule zinaboreshwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Meck Sadiki amesema kuwa wanatambua mchango wao na kuwa
watakuwa wamesaidia jitihada za serikali katika kupunguza changamoto za
madarasa.
Amesema
kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unakabiliwa na changamoto ya madarasa na
madawati hivyo kunahitaji wadau kujitokeza kusaidia maeneo hayo.
Mwenyekiti
wa TATOA, Angelina Ngalula amesema kuwa wameunga mkono jitihada za
serikali kwa upande wa elimu hivyo wanawajibu wa kufanya hivyo katika
kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa.
Amesema
kwa kuanzia wanaanza na madarasa 12 lakini wataendelea kuwasiliana na
wanachama zaidi katika kuongeza au kujenga shule nzima ili watoto wasome
shule na kuja kuweza kutumikia sekta ya usafirishaji.
Angelina
amesema kuwa bodi yao iko imara katika kwenda na suala la shule za
msingi ili watoto wapate elimu bora kutokana na mkakati wa Rais kutoa
kipaumbele ya elimu ya nchini.
No comments:
Post a Comment