TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, March 11, 2016

JUMUIYA YA KIMATAIFA YAKARIBISHA UTEUZI WA MKAPA YATAKA APEWE USHIRIKIANO


Na Mwandishi Maalum, New York
Jumuiya  ya Kimataifa  imezitaka pande zinazopinga  Nchi  Burundi, kumpatia ushirikiano wa  kutosha ,Rais  Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuratibu   majadiliano ya kutafuta  ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa   unaoendelea nchi humo.
Pamoja na  pande zinazopingana kutakiwa kufanya hivyo kwa moyo mmoja,  pia     Taasisi za Kimataifa na Kikanda  ukiwamo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, pamoja na wadau wengine wametakiwa pia kumuunga mkono na kutoa ushirikiano kwa Rais Mstaafu  Benjamin Mkapa.
Wito huo umetolewa siku ya Jumatano, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  wakati  Wajumbe wa    Burundi Configuration  walipokutana katika kikao chao  na kujadili hali ya kisiasa na kiusalama inavyoendelea nchi Burundi kufuatia ziara  iliyofanywa na  Mwakilisji wa Kidumu wa……  Balozi Jurg Lauber ambaye ni   Mwenyekiti wa   Burundi  Configuration.
“Tunakaribia  uteuzi wa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa kuwa  mratibu wa mazungumzo  ya  kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi. Tunatoa wito kwa pande zinazopingana nchi  humo, serikali na  vyama vya kiasa kumpatia ushirikiano bila ya mashari yoyote” akasema Mwakilishi wa Marekani.
Naye Mwakilishi  wa Kudumu wa  Ubeligiji, Balozi Benedicte Frankinet. Pamoja na kueleza kwamba   ujumbe wake   unawasiwasi kuhusu  taarifa za kuendelea kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mbinyo kwa vyombo vya habari na uhuru wa watu  kutembea.
Amesema .“ Rais Mstaafu wa Tanzania , Benjamin Mkapa, anauzoefu mkubwa na wa hali ya juu katika   uratibu na  utafutaji ufumbuzi wa  migogoro ya kisiasa, ujumbe wangu unakaribisha uteuzi wake, hapana shaka ataratibu  na kusimamia  majadiliano jumuishi  yatakayohusisha wadau wote wanaopingana  nchini Burundi wakiwamo pia wajumbe wa asasi zisizo za kiserikali”.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa  Kudumu wa  Netherland,  Balozi Karel Van Oosterom,  amesema ujumbe wake pia  unakaribisha uteuzi wa  Rais Mkapa, na kwamba pande zinazopinga nchini Burundi zinatakiwa kuitumia  fursa ya  uteuzi wa Mkapa kurejea katika  meza  ya majadiliano  ambayo  yatakuwa  jumuishi na  huku akizisihi pande hizo kutotoa masharti ya aina yoyote ile.
Naye   Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda,  pamoja na  kukaribisha  uteuzi wa Rais Mstaafu Mkapa ambaye amesema ana uzoefu mkubwa na wanaimani naye,  alimshukuru pia, Rais  John Pombe  Magufuli  kwa  kumteua Mkapa.
Karibu wajumbe wote waliochangia majadiliano kuhusu  hali ya  Burundi walikaribisha na kupongeza uteuzi wa Mkapa  huku, Mjumbe wa Nigeria pamoja  naye kuunga mkono uteuzi wa Mkapa.  Alisisitiza pia kwamba Majadiliano jumuishi ya kutafuta ufumbuzi wa  kudumu nchini  Burundi  yanapashwa kumilikiwa na Warundi wenyewe.
Akatahadharisha kwa kusema kwamba,   mashinikizo kutoka nje ya Burundi  hayana nafasi  katika  mchakato huo na kwamba hali  hiyo ikiruhusiwa inaweza  siyo tu kuathiri majadiliano hayo lakini pia  itakuwa ni kuwaingilia wananchi wa Burundi.
Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania,  Balozi Tuvako Manongi akichangia  majadiliano hayo, yeye ametaka ushughulikiaji wa  hali tete ya kisiasa na kiusalama uende sambamba na  uondoajji wa vikwazo  vya kiuchumi   kwa Serikali ya Burundi.
“  Hakuna  matinki ya kutia msisitizo wa  kuitaka serikali ya  Burundi kutekeleza mambo kadha wa kadhaa yakiwamo ya  ukiukwaji wa haki za binadamu, pasi kuzungumzia hali  mbaya  ya uchumi na kijamii  inayoikabili Burundi na watu  wake. Akasema Balozi
Nakusisitiza . “Tunapojadili hali ya  usalama tujadili  basi na uondoaji wa  vikwazo vya  kiuchumi kwa sababu mambo haya yanakwenda kwa  pamoja.  Njia sahihi ya kusaidia mchakato  wa  kutafuta amani ya  kudumu nchini Burundi ni kwa   sisi sote   tulio katika meza hii  kufanya kazi  kwa  pamoja  na  katika  namna  inayoeleweka”.
Vile vile Balozi Manongi ambaye Tanzania ni  mjumbe wa Burundi Configuration ambayo ni sehemu ya Kamisheni ya Ujenzi wa Amani ( Peace Building Commission)  amesisisiza  wananchi wa Burundi kumiliki   mchakato wa majadiliano kuhusu mustakabali wa nchi yao.
Hoja ya  kuondolewa kwa vikwazo vya  kiuchumi, Warundi kumiliki majadiliano yao, pia  imeungwa mkono  na  mjumbe wa China ambaye  amesema Haki za binadamu  zinahusu pia haki ya kupata maendeleo na kwamba Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kuisadia Burundi kiuchumi ili wananchi wapate  maendeleo ambayo ni haki yao.
www.shaabanmpalule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment