Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Geita Manzie
Mangochie anasema Tamasha la Pasaka ni
jambo kubwa sana kwao kwa sababu linafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.
Mangochie anasema ukubwa na
umuhimu wa tamasha hilo ni kutajwa kwa neno la Mungu na waimbaji sambamba na
viongozi mbalimbali wa dini wanaofika katika tamasha hilo.
Mangochie anasema Mkoa wa
Geita una matatizo mengi ambayo yalikuwa
yanahitaji kukemewa, lakini mwaka huu Mungu amesikia matakwa ya wakazi wengi wa
mikoa hiyo ambayo ilitawaliwa na matukio ya mauaji yakiwemo ya vikongwe na walemavu wa ngozi ‘Albino’.
“Mikoa hii ya Kanda ya ziwa
iligubikwa na shetani ambaye ni mauaji ya Maalbino na Wakongwe ambao walikuwa
wakitendewa unyama ambao Mungu alikuwa akichukizwa nao, hivyo kupitia Tamasha
la Pasaka neno la Mungu litasaidia kuondosha madhila hayo,” alisema Mangochie.
Mangochie anasema kupitia
Tamasha la Pasaka waandaaji watasaidia wakazi wa mikoa hiyo kuachana na kusahau
matukio ya kumchukiza Mungu.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha
hilo yanaendelea vilivyo kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa
jamii.
Msama alisema tamasha hilo
linatarajia kuanza Machi 26 kwenye ukumbi wa Desire ulioko mkoani Geita, Machi
27 litafanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na Machi 28 litafanyika
kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
Msama alisema viingilio kwa
wakubwa ni shilingi 5000 na watoto shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa wakazi
wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment