Na Zuena Msuya, Dar
Es Salaam
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II
chenye uwezo wa kuzalisha megawati 240 unaotokana na gesi asilia iliyogundulika
nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo,Rais Dkt Magufuli
anatarajiwa kuweka jiwe la msingi wiki ijayo
machi 16, na ujenzi wa mradi huo umeanza
mwezi Machi mwaka huu na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi
28.
Prof. Muhongo alifafanua kuwa mwanzoni mwaka 2018
,kituo cha Kinyerezi II kitaanza kuzalisha umeme wa megawati 240 ambapo kati ya
hizo megawati 180 zitatokana na Gesi asilia na megawati 60 zitatokana umeme
utakaozalishwa kutokana na joto litakalotokana na kuendesha mitambo ya kituo hicho.
" Mtambo huu ni wa kisasa zaidi kwani hakuna
kitakachopotea lile joto litakalokuwa linatoka kutokana na kuendehsa mashine
litazalisha umeme , tofauti na ilivyokuwa kwa Kinyerezi I ambapo joto hupotea
bure," alisema Profesa Muhongo.
Alisema kuwa kituo hicho kitagharimu Dolla za Kimarekani
milioni 344 hadi kukamilika kwake na tayari Mkandarasi atakayejenga kituo hicho amekwisha lipwa
fedha zake ambazo ni fedha kutoka Serikali ya Tanzania na mkopo wa bei nafuu kutoa Serikali ya Japan.Pia Profesa Muhongo alitumia ziara hiyo kuuleza
umma kuwa kwa sasa Serikali inaondokana
na miktaba ya malipo ya ziada ya mtaji
kwa kampuni zinazoiuzia umeme (TANESCO) ( Capercity charge) kwa mikataba
mipaya .
Sambamba na hilo alisema kuwa kinachofanyika sasa
ni kupitia upya mikataba iliyopo na kufanya mazungumzo na kampuni husika ili
kuondoa gharama zisizo za lazima.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Felchesim Mramba alisema mwishoni mwa mwezi huu
kituo cha umeme cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I kitaongeza uzalishaji wa
umeme wa megawati 80 na hivyo kufanya kituo hicho kuzalisha jumla ya megawati
150 kama inavyokusudiwa.
Mramba aliongeza kuwa mwanzoni mwa mwezi April, Mkoa wa Dar es
salaam , utakuwa unapata umeme moja kwa moja kutoka Kinyerezi I tofauti na
ilivyokuwa hapo awali ilikuwa ikitegemea kupata umeme kutoka kituo cha ubungo
pekee.
Mramba alisema kukamilika kwa kiasi hicho cha
umeme kutapunguza kabisa tatizo la kukakatika umeme mara kwa mara nchini.Katika ziara hiyo Profesa Muhongo alitembelea
Kituo cha umeme cha City Center pamoja na cha Mikocheni ambavyo vitaliwezesha
jiji la Dar es salaam kuondokana na nyaya za umeme zinazopita juu.
Akimfafanua waziri Mhongo meneja mwandamizi wa miradi
ya usafirishaji na usambazaji Mhandisi Gregory Chegere, alisema miundombinu ya
umeme ya katika kituo hicho itapita chini ya ardhi na hivyo kuondoa adha ya
kukata miti pamoja na kuangushwa kwa nguzo kutokana na mvua zitakazokuwa
zinanyesha kwa jiji la Dar Es Salaam.
Mhandisi Chegere alisema kituo hicho kitaanza kazi
mwezi April na kuuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kuwa na umeme wa uhakika na
usiokatika.
No comments:
Post a Comment