TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 7, 2016

MFANYABIASHARA WA UTALII ARUSHA ATOA MISAADA YA KIJAMII HOSPITALI MKOA WA ARUSHA LEO. MTAZAME RAIS MAGUFULI AKIMTANGAZA KATIBU MKUU MPYA IKULU JIJINI DAR Kichupa cha leo #LETIGO by Nameless and Nyashinski WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA MKOANI SIMIYU MWAMBATA WA ZAMANI WA JESHI UBALOZI WATANZANIA NCHINI MAREKANI NA CANADA BRIGADIEAR GENERAL EMMANUEL MAGANGA ASTAAFU RASMI CATHERINE MAGIGE AKARABATI OFISI YA UWT MKOANI ARUSHA RAIS MAGUFULI AMTEUA BALOZI JOHN WILLIAM KIJAZI KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWAHUTUBIA WANAWAKE KWENYE MAADHIMISHI YA KIMATAIFA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI DKT. SHEIN AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MZEE HAMID AMEIR MUASISI WA MAPINDUZI RAIS WA VIETNAM KUFANYA ZIARA YA KWANZA YA KITAIFA NCHINI VIJIMAMBO INAKUTAKIA JUMAPILI NJEMA NA UPENDO NKONE- HALELUYA USIFIWE HAPPY BIRTHDAY UDSM YAKANUSHA TAARIFA ZA KUWANYANYASA WATUMISHI WAKE CHUO KIKUU CHA MZUMBE CHAPONGEZWA KWA KUIMARISHA ELIMU NCHINI DAR USIKU, UNAWEZA KUDHANI UKAHABA UMEHALALISHW IKULU YAVUNJA UKIMYA SAKATA LA UMEYA DAR CHADEMA YACHAMBUA SIKU 120 ZA MAGUFULI VIDEO: LULU NA RICHIE WASHINDA TUZO ZA AMVCA 2016 MAONESHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MNARA WA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI KISONGE ZANZIBAR MAGAZETI YA MARCH 06, 2016 SHEREHE YA RED CARPET DAY SEATTLE WA. Bocco avuruga chereko Yanga Chadema Monduli yamkubali Magufuli Mama afariki dunia pamoja na watoto wake wachanga kwa kukosa damu













Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Stendi mjini Mwanhuzi. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SERIKALI imeanzisha mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali  katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa  

Waziri Mkuu alisema mfumo huo unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha  taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja na hadi anapostaafu.

Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, maafisa utumishi walipaswa kukusanya taarifa za watumishi wote walioajiriwa na kuzipeleka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili zikathibitishwe kabla ya kuzipeleka HAZINA kwa maandalizi ya mishahara. 

Akitolea mfano wa kada ya ualimu, Waziri Mkuu alisema ajira za walimu zilikuwa zinaanzia Idara ya Utumishi wa Walimu  (TSD)  lakini anapaswa aende kuripoti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  (DED) ambaye ni mwajiri wake chini ya TAMISEMI. "Hii ilileta ugumu wa malipo ya kupanda madaraja, uhamisho ama likizo kwa sababu mwajiri anakuwa hajatenga hizo fedha."


"Sasa hivi tuna Tume ya Utumishi wa Walimu  (TSC) ambayo iko chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Kwa hiyo ni rahisi wao kukaa pamoja na kuamua tuwapandishe daraja walimu 10 na wote hao wakalipwa bula bila kuchelewa," alisema.


Alisema mfumo huo umeanza kutumika tangu mwaka 2012 na ulianza kwa ajira mpya za wakimu na hadi sasa umethibitisha kuwa inawezekana kumlipa mtumishi mshahara wake hata kama ameajiriwa ndani ya mwezi huohuo.


"Kama mtumishi anaripoti kwenye kituo kipya hata iwe wilaya ya wapi ili mradi amefika na barua zake zote na ziko sahihi mtu huyu ataingiziwa taarifa zake na wakati huohuo taarifa zitaonekanaOfisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na pia zitapokelewa kwa maafisa wanaoshughikia mishahara kule HAZINA."

Alisema changamoto pekee waliyokutana nayo wakati mfumo huo umeanza ilikuwa ni kutoingizwa taarifa za wale ambao wameripoti baada ya tarehe 10 ya mwezi husika. "Hii ni kwa sababu matayarisho ya mishahara yanakuwa yameshaanza. Kwa hiyo wengi walishauriwa kuripoti kati ya tarehe 25 hadi tarehe 9 ya mwezi uliofuata na wote hawa hawakupata matatizo ya kucheleweshewa mshahara," alisema.


Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema  Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya. "Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara  na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua hiyo hiyo " alisema.


Wakati huohuo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelazimika kukatisha ziara ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa imalizike kesho kutokana na msiba wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo alipangiwa kuitembelea leo.

Mkurugenzi huyo Bw. Traceas Kagenzi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na shinikizo la damu. 

Atasafirishwa kwenda Muleba  kwa mazishi.


Akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya kumuombea marehemu Kagenzi iliyofanyika nyumbani kwake Maswa mjini, Waziri Mkuu alisema ameshtushwa na msiba huo uliotokea ghafla na kwamba Taifa limempoteza mtumishi mahiri ambaye bado Taifa lilikuwa likimtegemea.


"Nimeshtushwa sana na taarifa za msiba huu. Nimeambiwa hadi juzi usiku alikuwa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hii kuandika taarifa ya ziara ya wilaya hii. Kwa niaba ya Serikali, ninawapa pole sana wafiwa na Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi," alisema.


"Nimelazimika kukatisha ziara ya mkoa huu kwa sababu huyu ni mtumishi mwenzetu.
\
Mwambata jeshi wa zamani nchini Marekani na Canada Brigadier General Emmanuel Edward Maganga siku ya ijumaa trh 04 March alikuwa miongoni mwa majenerali 16 walioagwa rasmi baada ya kustaafu utumishi jeshini. Jenerali Maganga amestaafu akiwa na wadhifa wa Mkaguzi Mkuu wa Jeshi. Amelitumikia jeshi kwa takriban miaka 37 na mwezi mmoja. Katika utumishi wake zaidi ya kuwa Mwambata jeshi USA na Canada pia aliwahi kuwa Mwambata Jeshi nchini Africa ya Kusini akiwa pia analiwakilisha jeshi katika nchi za Angola, Botswana,Lesotho na Namibia. Watanzania walioko Marekani watakumbuka upendo wake kwao akiwa na mke wake Untie Love na ushiriki wao usiobagua katika matukio ya raha na shida. Timu ya VIJIMAMBO inamuombea maisha mapya ya furaha na kumkaribisha URAIANI. Hongera SANA Kamanda, mwanataaluma ya uandishi wa habari, mwanadiplomasia, mwanamikakati, Mkaguzi uliyebobea na mwanamichezo madhubuti.
Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige, leo amekabidhi ofisi ya UWT mkoa wa Arusha ambayo amefanyia ukarabati na kuweka vitu vya thamani iliyogharimu shilingi milioni 6 na nusu.
Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige akicheza ngoma na viongozi wa UWT mkoa wa Arusha mara baada ya kukabidhi ofisi ya UWT aliyokarabati kwa gaharama ya shilingi milioni 6.5 ,ambapo ofisi imepakwa rangi ,kuwekwa tiles , viti, meza , amakabati pamoja na TV.
Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa UWT mkoani Arusha.



Bi. Mindi Kasiga naye akitolea ufafanuzi ratiba nzima ya ziara ya Rais huyo wa Vietnam.
Sehemu nyingine ya waandishi wa Habari wakinukuu baadhi ya pointi wakati mkutano ukiendelea. Picha na Reginald Philip

Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang atakuwa Rais wa kwanza kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Rais Sang atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere siku ya Jumanne tarehe 08 Machi 2016 saa mbili usiku na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ambapo mapokezi rasmi yatafanywa siku ya pili na mwenyeji wake, Rais Dkt. Magufuli katika Viwanja vya Ikulu.

Akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake leo, Waziri Mahiga alieleza kuwa Rais Sang atafutana na mke wake, Mama Mai Thi, Mawaziri watano na Wafanyabiashara 51 katika ziara hiyo. Dkt. Mahiga alieleza kuwa Serikali inaupa uzito wa pekee ugeni huo kwa sababu ni ziara ya kwanza ya kitaifa katika Awamu ya Tano kufanywa na Mkuu wa Nchi. “Wakuu wa Nchi kadhaa walishakuja hapa nchini lakini kwa ziara za kikazi, sio za kiserikali, hivyo Vietnam imetupa heshima kubwa sana”. Waziri Mahiga alisema.

Rais Sang ni mara ya kwanza kufanya ziara katika Bara la Afrika na Tanzania ambapo pia atazuru nchi ya Msumbiji baada ya kuondoka hapa nchini tarehe 11 Machi 2016.

Dkt. Mahiga aliwambia Waandishi wa Habari kuwa Tanzania ina mambo mengi ya kujifunza kutoka Vietnam namna ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo katika kipindi kifupi, licha ya kuendesha vita kubwa ya mapambano ya kupigania uhuru dhidi ya Ufaransa na baadaye dhidi ya Marekani. Alisema nchi hiyo imepiga hatua katika sekta za viwanda, kilimo, mawasiliano na uvuvi. Kwa upande wa kilimo, nchi hiyo ni ya kwanza kwa kuuza kahawa aina ya robusta na korosho duniani ingawa mbegu za mazao hayo zimechukuliwa Tanzania. 

Aidha, Vietnam ni maarufu duniani kwa kuuza samaki aina ya sato ambao walichukuliwa kutoka Ziwa Victoria.

Waziri wa Mambo ya Nje alieleza kuwa ili Tanzania nayo ifike ilipo Vietnam ni lazima ifuate mambo matatu ambayo Vietnam inayazingatia. Mambo hayo ni kufanya kazi kwa bidii katika mazingira ya aina zote, utekelezaji wa maamuzi wanayofanya na kuwekeza katika mafunzo ya ufundi, miundombinu kama ya umeme, barabara, reli, bandari na mabemki kwa ajili ya mitaji na huduma nyingine za kifedha.

Katika ziara hiyo, Rais wa Vietnam pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake; Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein; Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai; Kuongea na wafanyabiashara na kutembelea eneo la uwekezaji la EPZA, Ubungo Jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment