Na Dotto Mwaibale
WAKALA
wa Majengo Tanzania (TBA), umecharuka kwa kuingia mkataba na Kampuni
ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd ili kusaidia kukusanya
madeni ya wadaiwa sugu ambao walikopa nyumba.
Wakati
huo huo mwakilishi wa kampuni hiyo ya udalali ya Yono Auction Mart
& Co. Ltd, Scollastica Kevela ametoa siku tatu kwa wadaiwa wote wa
TBA kuhakikisha wanalipa fedha hizo kabla ya kufikiwa na kampuni hiyo
ambayo Jumatano ya Machi 16 mwaka huu itaanza rasmi kazi ya kuwaondoa
katika nyumba za wakala huo watumishi wote wanaodaiwa kwa kufuata sheria
kama inavyoelekeza.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa
kutiliana saini na kampuni hiyo ya udalali kwa ajili ya kukusanya fedha
kutoka kwa wadeni wa wakala huo Mtendaji Mkuu wa TBA , Elius
Mwakalinga alisema wamefia hatua hiyo baada ya kuona wadaiwa wao ambao
wengi wao ni kutoka sekta za serikali kushindwa kulipa fedha hizo.
"Tumeingia
mkataba na Kampuni ya Yono Auction Mart baada ya kushinda zabuni ambayo
tulitangaza Februari 23,2016 na sasa kazi yote ya ukusanyaji wa fedha
hizo itafanywa na kampuni hiyo" alisema Mwakalinga.
Mwakalinga
alisema fedha nyingi za wakala huo zipo mikononi mwa wadaiwa wao ambapo
kwa mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma ni shilingi.Bilioni 6 na kwa
waliokopa ni sh.milioni 800 huku fedha zinazodaiwa kwa ajili ya kutoa
ushauri mbalimbali wa ujenzi ni sh.bilioni 6.95.
Mwakilishi
wa kampuni ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela
alisema wametoa siku tatu kwa wadaiwa wote kuhakikisha wanalipa fedha
hizo vinginevyo watafikiwa na kampuni hiyo ambayo imepanga rasmi kupita
kila nyumba inayodaiwa na kuwa kila muhusika atatakiwa kuilipa kampuni
hiyo asilimia tano ya fedha anazodaiwa na TBA.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) , Arch. Elius Mwakalinga
(kushoto), akikabidhiana hati ya mkataba na Mwakilishi wa Kampuni ya
Udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela Dar es
Salaam leo asubuhi, baada ya kampuni hiyo kushinda zabuni ya kukusanya
madeni ya TBA kuanzia leo.
Taswira meza kuu katika mkutano huo.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) , Arch Elius Mwakalinga
(katikati), akizungumza katika mkutano huo kabla ya kutiliana saini na
kampuni ya Yono. Kushoto Ofisa wa Idara ya Manunuzi, Mariam Kazoba.
No comments:
Post a Comment