- MKWASA ATANGAZA KIKOSI CHA WACHEZAJI 25 KUWAVAA CHAD
- BALOZI SEFUE: HII NI SERIKALI YA MABADILIKO
- Mkaguzi wa Ndani abaini uozo zaidi Jiji la Arusha
- Waziri aahidiwa rushwa ya Sh5 bilioni
- UNDP WAFANYA KONGAMANO LA VIJANA, LENGO NI KUWASAIDIA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI
- Maalim Seif apumzishwa Hospitali ya Hindu Mandal
- Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Pili wa Vyama vya Kijamii vya ICGLR
- Wasira amng’ang’ania Bulaya
- Waziri Mahiga ashiriki ibada ya kumuaga Marehemu Balozi Rwegasira
- SHUGHULI YA MAWLID YA KUMSIFU MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W) SIKU YA 19/03/2016 SEGEREA MWISHO,DAR
- VIDEO: MSAADA KWA NDUGU YETU AHMED ALBAITY UNAHITAJIKA
- Siri za Balozi Sefue kung’oka Ikulu
- SERIKALI YAZISHAURI TAASISI ZA KIBENKI NCHINI KUWA NA VILABU VYA MICHEZO NA MASHINDANO
- VOTING IS OPEN FOR 2016 DICOTA AWARDS
- Mrembo Hair LLC
Posted: 08 Mar 2016 10:27 AM PST
|
||
Posted: 08 Mar 2016 09:53 AM PST
|
||
Posted: 08 Mar 2016 09:51 AM PST
Ningependa
kutumia fursa hii kama Dada, Mke, Mama, mfanyakazi, Mwanaharakati na
mjasiliamali kuwapongeza wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu
ya kuwaenzi wanawake wote ulimwenguni.
Historia
ya Maisha yangu, ni kielelezo cha maisha ya wanawake wengi ulimwenguni
wanaopitia changamoto mbalimbali. Nililelewa katika mazingira kandamizi
ya Jinsia ya kike-kwenye jamii ambayo mtoto wa kiume alipewa nafasi ya
kipekee katika masuala mbalimbali dhidi ya mtoto wa kike...Kwa mfano
kipaumbele cha kupata elimu walipewa watoto wa kiume wakati watoto wa
kike wakitarajiwa kushughulika na kazi za nyumbani, kupika,kuchota maji
na kusaidia shughuli za kilimo na hatimaye kuolewa.
Bibi
yangu (Apumzike kwa Amani) alikuwa mhanga wa mfumo huo kandamizi. Kwa
taabu alizopita Bibi yangu alijiwekea nadhiri kwamba Mjuu wake,
hatopitia shida alizopitia yeye...na hivyo siku zote alikuwa akiniasa
kwamba "Niyu (jina langu la nyumbani),Unaweza kila kitu kinachofanywa na
mtoto wa Kiume". Aliniimarisha kifikra na kiakili.
Na
siku zote alikuwa na msemo wake "Niyu Kasome, Ukasome umshinde Babu
yako, Usije kuwa unanyanyasika kama sisi"- ushauri wake ndio ulikuwa
dira yangu ya maisha ambapo nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuhitimu
shahada ya uzamili katika masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha
Strathclyde cha Uingereza.
Hadi
hivi leo, sauti ya Bibi haijakoma masikioni mwangu, sijaacha kutafuta
elimu na maarifa ya masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo katika
jamii...ni kwa sababu hiyo nilipata mafunzo ya muda mfupi ya uongozi na
majadiliano kutoka Chuo kikuu cha Harvard cha nchini Marekani.
Nitaendelea kuitafuta Elimu na pia kusaidia wenzangu, sababu naamini
moja ya njia ya Mwanamke kujikomboa katika ukandamizaji wa kijinsia ni
kuongeza kiwango cha elimu kwake mwenyewe na kwa wanawake wenzake.
Waswahili
wana msemo usemao maisha ni shule.....msemo huu nimeuishi katika maisha
yangu ya baada ya masomo. Nimefanya kazi katika mashirika mbalimbali
yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi. nimefanya kazi na taasisi ya ISHI
iliyokuwa inashughulikia masuala ya Ukimwi, baada ya hapo nimefanya pia
katika kampuni ya Philips Medical Systems ya Uholanzi na baadaye
nimefanya kazi kampuni ya mawasiliano ya Maktech. Kwote nilipopita
nimekumbana na changamoto mbalimbali zilizohusiana na jinsia yangu.
Utekelezaji
wa majukumu yangu ulinilazimu kuwa na mikutano na watu mbalimbali
Serikalini na kwenye taasisi za fedha ambapo watu niliokuwa nakutana nao
ni wanaume ambao baadhi yao wamekuwa na mawazo ya mfumo dume yaliyojaa
dharau na manyanyaso. Wengine kwenye fikra zao wanadhani mwanamke yeyote
mwenye mafanikio, iwe kwenye biashara, siasa, ajira, lazima anabebwa na
wanaume. Wakiona mwanamke amefanikiwa tu, utasikia..huyu 'hawala wa
fulani'. hii ni dhana potofu na inayolenga kumdhalilisha na kumnyanyasa
mwanamke. Mimi binafsi sikukubali kuyumbishwa na watu wenye mawazo ya
aina hiyo.
Kila
nilipokumbana na changamoto za aina hiyo nilipata hamasa ya kufanya
kazi kwa bidii zaidi na kuwadhihirishia kwamba NINAWEZA, ilee sauti ya
bibi ndioa ilikuwa ikinitia hamasa zaidi na zaidi na hatimaye
kuniwezesha kufanya vizuri hadi kufikia kuaminiwa kupewa majukumu
makubwa zaidi kama vile Mkurugenzi Mkuu katika kampuni ya Mokasi Medical
Systems ambayo ni wakala wa kampuni ya Philips ya Uholanzi. Hasama hiyo
iliniwezesha pia kuanzisha kampuni yangu inayotoa Huduma za kifedha -
Monfinance Investment Group Ltd.
Mbali
na shughuli hizo nimeweza pia kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya
wakurugenzi ya FINCA Microfinance Tanzania. Kwa ujumla siku zote za
maisha yangu nimejihusisha na harakati za kupigania haki za wenye shida
na mahitaji katika jamii kutokana na msingi niliojengewa na bibi yangu
wa kukataa unyonge na kusaidia wanyonge. Hurka hiyo ndio ilipelekea
ajira yangu ya kwanza kuwa kwenye taasisi ya uhamasishaji wa masuala ya
ukimwi ya ISHI. Niliguswa kujihusisha na kampeni hizo kwasababu binafsi
nimepoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na ugonjwa huo. Mbali na
ISHI,nimekuwa nikijihusisha na kampeni ya kuzuia mauaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi (Albino) iitwayo IMETOSHA.
Ni
jambo la udhalilishaji uliopitiliza kuwakata binadamu wenzetu viongo
vyao kwa imani za kishirikina. Pia nimeshiriki kwenye uhamasishaji wa
magonjwa yasiyojulikana (Rare diseases). Tunaposherehekea siku ya
Mwanamke duniani rai yangu kwa wanawake wenzangu, tushirikiane,
tusaidiane, tupeane moyo na tuwezeshana ili tufikie lengo letu la usawa
50/50 kufikia mwaka 2030. Kila mwanamke atimize wajibu wake kwa
kujitambua na kuhakikisha haki yake hainyongwi.
Mimi
nimejitambua, ninasimamia haki yangu, na wala siipiganii, ni yangu,
Jinsia yangu hainitofautishi kiutendaji na jinsia ya kiume.
Ninachoangalia ni Mchango wangu katika maendeleo ya Uchumi, jamii na
familia na sio Jinsia yangu. Ninachotambua katika jinsia yangu ni kuwa
mimi ni Dada, Mama, rafiki, na Mke. Mengine yote,nipo sawa na wote,
wanaume na wanawake. Happy Women's Day 2016.
"Wanawake
Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima". Women
should view their gender as a resource rather than a liability) - MJ.
|
||
Posted: 08 Mar 2016 08:57 AM PST
Mkurugenzi
wa Takwimu za Sensa na Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim
Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi
Februari, 2016. Kulia ni Meneja Idara ya Ajira na Bei, Ruth Minja.
Wapiga picha wakiwa kazini.
Na Dotto Mwaibale OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei katika Februari mwaka huu umepungua mpaka kufikia asilimia 5.6 kutoka asilimia 6.5 ya mwezi Januari. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Mkurugezi wa Sensa za Jamii, Ephraim Kwesigabo alisema kasi ya upunguaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka huu kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi za vyakula na bidhaa zisiyakula kwa kipindi kilichoishia cha Februlia, 20 ikilinganishwa na bei za Februari mwaka 2015. Alisema kuwa mfumuko wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Februari mwaka huu umepungua kwa asilimia 10.3, mafuta ya dezeli kwa asilimia 4.5 na matunda kwa asilimia 7.2. Kwesigabo alisema pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kuna baadhi ya bidhaa zinaonyesha kuongezeka katika hicho ni pamoja na Sukari kwa asilimia 7.1, Mkaa asilimia 4.3, Mchele kwa asilimia 22.9 na viazi 16.3. Aidha alisema hali ya mfumuko wa bei katika nchi za jilani unaelekea kufanana na nchi za afrika mashariki ambapo Kenya umepungua hadi asilimia 6.84 kutoka asilimi7.78 mwaka huu, Uganda umeongezeka kwa asilimia 7.7 kutoka asilimia 7.6 kwa mwezi Januari mwaka huu.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
|
||
Posted: 08 Mar 2016 08:42 AM PST
Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (katikati) akimkabidhi
sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali Caroline Hanne Van, Raia wa Denmark
kwa niaba ya watoto wawili (kitandani) waliodaiwa kuokotwa jana maeneo
ya Mbezi Beach na kufikishwa hospitalini hapo leo asubuhi, wakati
Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa
msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo Machi 8, 2016.
Kushoto ni Emel Kudahl Christensen na wa tatu (kulia aliyekaa) ni Emma
Nikoline Wennberg, wauguzi wa kujitolea kutoka nchini Denmark.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa vitu mbalimbali
kwa wagonjwa wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya Watoto wachanga/Njiti,
wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya
kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa vitu mbalimbali
kwa wagonjwa wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya Watoto wachanga/Njiti,
wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya
kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa vitu mbalimbali
kwa wagonjwa wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya Watoto wachanga/Njiti,
wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya
kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Meneja
wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (kulia) akimkabidhi sehemu ya
msaada wa vitu mbalimbali mzazi aliyejifungua mtoto wa Kiume, Hospitali
ya Mwananyama, Joyce Lucas, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam,
wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya
kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Meneja
wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (kushoto) akikabidhi sehemu ya
msaada wa vitu mbalimbali kwa wazazi waliokuwa wamelazwa kweye Wodi ya
Watoto wachanga/Njiti katika Hospitali ya Mwananyama, wakati
Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa
msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Meneja
wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (kulia) akimkabidhi sehemu ya
msaada wa vitu mbalimbali mgonjwa mzazi aliyelazwa kwenye Wodi ya kina
mama waliofanyiwa upasuaji Hospitali ya Mwananyama, jijini Dar es
Salaam, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa
ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni
sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya Kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (wa pili kulia) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janet Ezekiel, wakiwaangalia watoto wawili waliodaiwa kuokotwa maeneo ya Mbezi Beach, waliofikishwa Hospitali ya Mwananyamala.
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Wafanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Picha ya pozi ......
Picha ya pozi na mtoto.....
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Mfanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa
wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya kinamama, wakati Wafanyakazi wa Mfuko
huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakisubiri kuingia wodi ya wazazi wa upasuaji kugawa msaada wa vitu mbalimbali leo.
Wafanyakazi hao wakipozi na baadhi ya vitu walivyoshusha kwenye magari yao kabla ya kuanza zoezi la kugawa.
Wafanyakazi hao wakiendelea kushusha vitu hivyo kutoka kwenye magari...
Wafanyakazi hao wakiendelea kushusha vitu hivyo kutoka kwenye magari...
Meneja
wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko huo baada ya zoezi la kugawa vitu
hivyo leo kwenye Hospitali ya Mwananyamala.
|
||
Posted: 08 Mar 2016 07:52 AM PST
Mazoezi
yataanza sooner kujiandaa na mechi ya Yanga na Simba Memorial
Weekend hapa hapa New york. Hiyo ni nafasi ya wapenzi wa Yanga na Simba
kutoana jasho na Kombe uwanjani siku hiyo mtoto hatumwi dukani kwani
akitumwa dukani change mali yake au itapotelea njiani kabisa kabla
kufika nyumbani. Tafadhani tafadhali ukisoma hii habari mwambie mnazi
mwenzio kuwa awile mwana siku hiyo.
|
||
Posted: 08 Mar 2016 05:08 AM PST
Siku
chache baada ya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza
zuio la uingizwaji wa bidhaa ya sukari kutoka nje ya nchi, leo March 8
2016 Serikali kupitia bodi ya sukari Tanzania, imetangaza viwango vipya
vya bei ya sukari nchini vitakavyoanza kutumika hivi karibuni, akiongea
na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry
Semwanza amesema.
Serikali,
kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya
rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja‘
‘wafanyabiashara
wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari
inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi‘
‘Maafisa
biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa
agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki
za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo‘
|
||
Posted: 08 Mar 2016 04:42 AM PST
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Profesa Choi Oe Chool Rais wa GLOBAL SAEMAUL DEVOLOPMENT
NETWORK ya Jamhuri ya Korea, Wakati Rais huyo na Ujumbe wake alipofika
Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March 08,2016, kwenye
mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia juu ya kukuza na kuendeleza
ushirikiano wa kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Uchumi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipokea ratiba ya mpango wa maendeleo wa Jumuiya ya GLOBAL SAEMAUL
UNDONG kutoka kwa Profesa Choi Oe Chool Rais wa GLOBAL SAEMAUL
DEVOLOPMENT NETWORK ya Jamhuri ya Korea, Wakati Rais huyo na Ujumbe
wake walipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March
08,2016, kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia juu ya kukuza
na kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali
ikiwemo Uchumi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya GLOBAL
SAEMAUL DEVOLOPMENT NETWORK ya Jamhuri ya Korea, Wakati Ujumbe huo
ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March
08,2016.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Ujumbe wa Uwekezaji katika Nyanja wa Viwanda vya Sukari
kutoka Kampuni ya RAK INTERNATIONAL LTD ya India, Wakati Ujumbe huo
ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March
08,2016, kwa lengo la kutaka kuwekeza Viwanda vya Sukari hapa Nchini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiangalia mpango wa maendeleo wa Viwanda ulioandaliwa na Kampuni ya RAK
INTERNATIONAL LTD ya India, Wakati Ujumbe wa Kampuni hiyo ulipofika
Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March 08,2016, kwa
lengo la kutaka kuwekeza Viwanda vya Sukari hapa Nchini. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya RAK INTERNATIONAL LTD Bw. Sundeep
Patil. (Picha na OMR)
|
||
Posted: 08 Mar 2016 03:24 AM PST
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia
ya Kilimanjaro Premieum Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangza
kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa
fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Chad, Machi 23, 2016 mjini
Djamena.
Akiongea
na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho, Mkwasa amewaomba
wachezaji aliowaita katika kikosi hicho, kujiweka fit katika mazoezi
wanayoyafanya katika vilabu vyao, kwani hakutakua na muda wa kufanya
mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.
“Ligi
Kuu ya Vodacom, michuano ya CAF (CL, CC) inachezwa wikiendi ya tarehe
18-20 Machi, hivyo wachezaji wote watakua na majukumu katiak timu zao,
muda wa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mchezo huo hautakuwepo,
ndio maana nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda
wenyewe kwa kuwa fit wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo wa machi 23,
2016” alisema Mkwasa
Wachezaji
walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula (Azam FC), Ally
Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi ni Juma
Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe,
Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).
Viungo
Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla,
Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa
Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).
Washambuliaji
ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe),
John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda
(Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba SC).
|
||
Posted: 08 Mar 2016 03:14 AM PST
Baada
ya kudumu Ikulu kwa takribani siku 127zikiwamo 67 tangu aongezewe muda
wa mwaka moja akiwa na Serikali ya Awamu ya Tano, Balozi Ombeni Sefue
ameshukuru heshima aliyopewa na Rais John Magufuli kwa muda wote
aliomsaidia kutekeleza majukumu yake ya ukatibu mkuu kiongozi na kueleza
kuwa Serikali ya sasa ni ya mabadiliko.
Wakati
Sefue akiondoka, mhandisi John Kijazi amepokea kijiti cha ukuu wa
utumishi serikalini na kuahidi kuwa atafuatilia mazingira ya watumishi
wote pamoja na mazingira yao, ili kurekebisha panapohitajika kwa lengo
la kuongeza uwajibikaji na tija kwa wananchi.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kuapishwa kwa mrithi wake, licha ya kumshukuru
Rais, Balozi Sefue aliwataka watendaji wote serikalini kumpa ushirikiano
wa kutosha Balozi Kijazi ili kuleta ufanisi kwenye huduma za umma.
“Namshukuru
Rais kwa kuniamini kwa kipindi chote nilichodumu naye. Ni heshima kubwa
kuwatumikia Watanzania pamoja naye. Nitampa ushirikiano wowote
atakaouhitaji katibu mkuu kiongozi mpya kwenye utekelezaji wa majukumu
yake,” alisema Sefue.
Rais
Magufuli, ameahidi na mara zote amekuwa akisisitiza adhma yake ya
kutumbua majipu kwa watumishi wote ambao hawaendani na kasi yake. Tangu
taarifa za mabadilio hayo zilipotangazwa jana, kumekuwepo na tetesi
nyingi kuwa huenda Sefue naye ni jipu lilikuwepo ikulu, suala ambalo
halikupata maelezo ya kutosha kutoka kwa balozi huyo.
Kwa
upande wake Kijazi, alisema atafanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya
Rais huku akimshauri namna sahihi za kuboresha mazingira ya utumishi
serikalini.
Akieleza
juu ya majukumu yake mapya, alionyesha kuyatambua ipasavyo na
kubainisha kuwa atashirikiana na Baraza la Mawaziri kwenye vikao vyao,
bila kusahau kuzifuatilia wizara husika na kuona endapo kila kitu
kinaenda kama inavyotakiwa.
“Nitakutana
na mawaziri kwenye vikao vyao nitakavyoviandaa. Nitawasiliana na
kuwafuatilia watendaji wa wizara husika juu ya masuala yatakayokuwa
yamejitokeza ndani ya maeneo yao ya uwajibikaji. Kila mmoja atimize
wajibu wake ili Taifa lisonge mbele,” alisema Kijazi.
Ili
kuitendea haki hadhi ya utumishi wa umma, Kijazi ameahidi kuhakikisha
kila kitu kinasimamiwa kwa ukaribu huku akitoa msisitizo kwenye
vipaumbele vya Rais. “Kwenye suala la mapato na rushwa, nitafuatilia kwa
nguvu ili kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa Serikali,” alisisitiza
Kijazi.
Balozi
Kijazi aliteuliwa juzi kushika nafasi inayoachwa na Balozi Sefue. Kabla
ya uteuzi huo, Kijazi alikuwa mwakilishi wa Tanzania kwa nchi za India,
Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal huku makazi yake yakiwa
jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007.
Katika
wadhifa huo, alikuwa mkuu wa mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje
ya nchi pamoja na mkuu wa mabalozi wa Afrika nchini India. Kabla
hajateuliwa kuwa mwakilishi wa nchi, Kijazi amekuwa mtumishi serikalini
kwa nafasi mbalimbali ikiwamo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi kuanzia mwaka
2002 mpaka 2006.
Kabla ya hapo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kati ya mwaka 1996 hadi 2002.
Ndani
ya Wizara ya Ujenzi, kabla hajawa katibu mkuu, alikuwa mhandisi
mwandamizi wa ujenzi wa barabara kisha kupandishwa cheo na kuwa
mkurugenzi wa barabara za mikoa.
Kumbukumbu
za taaluma yake zinaonyesha kuwa alipata Shahada yake ya kwanza ya
Sayansi ya Uhandisi wa Umma mwaka 1982 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, na baadaye Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Barabara kutoka
Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza mwaka 1992.
Jana
wakati anaapishwa, saa 4:15 asubuhi, Kijazi alikuwa sambamba na mke
wake, Fransiscar Kijazi na kwa pamoja wamejaliwa watoto watatu, David,
Emmanuel na Richard. Kwa heshima ya familia hiyo, baada ya kukamilisha
protokali, Rais Magufuli alipiga picha ya pamoja na familia ya mteule
huyo mpya atakayehudumu ikulu kuanzia sasa.
Hata
hivyo kwa mara ya mwisho, Sefue aliendelea na kazi yake mpaka jana
asubuhi na ndiye aliyemkabidhi Kijazi kitabu kitakatifu cha Biblia,
Katiba na kiapo cha uongozi ambacho alisaini.
Wadau wazungumza
Balozi
Abdul Faraji alisema mabadiliko yaliyofanyika ya katibu mkuu kiongozi
ni ya kawaida katika nchi mbalimbali ulimwenguni, hasa pale Serikali
mpya inavyoingia madarakani. Alisema kila Rais mpya mara nyingi hupenda
kuingia ofisini akiwa na timu ya watu wake, ambao anaona watafanikisha
utelekelezaji wa malengo aliyojiwekea katika Serikali yake.
Faraji
ambaye aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali duniani
ikiwamo Ufaransa (1972-1973), alisema balozi Sefue emeondoka Ikulu akiwa
amefanya kazi kubwa ambayo anatakiwa kupongezwa na kila Mtanzania.
“Tunamsifu kwa kazi yake hasa kwa kipindi hiki cha miezi mitatu ya
utawala wa Rais Magufuli. Alijitahidi kwenda na kasi ya mabadiliko kwa
uwezo wake ukizingatia alikuwa kwenye awamu ya Serikali ya awamu ya nne
ambayo siasa yake haikuwa na kasi kama ya sasa,” alisema.
Wakati
mijadala katika mitandao ya kijamii ikiendelea juu ya muda mfupi
aliokaa balozi Sefue, Mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shumbusho Damian alisema muda
huo huenda ulikuwa ni maalumu kumpatia uzoefu Rais Magufuli katika
masuala mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea Serikalini.
“Jambo
ambalo sikutegemea ni kumteua Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kwa
sababu nadharia iliyokuwepo ni kwamba Rais Magufuli anataka kufanya kazi
na watu wapya ambao hajawahi kufanya nao kazi”, alisema.
Katibu
Mkuu wa chama cha CCK, Renatus Muabhi alimpongeza Rais Magufuli kwa
uteuzi huo na kueleza kuwa ni wakati mwafaka kwa Serikali yake
kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wenye kashfa.
“Kila
utawala ni lazima uwe na safu yake ya uongozi ili kuondoa viraka
vitakavyokwamisha utekelezaji wa baadhi ya mambo yanayoletwa na mfumo
mpya. Rais alitwambia kuwa ameikuta nchi katika hali mbaya, hivyo ni
wakati muafaka wa kuwaondoa wote wenye tuhuma,” alisema Muabhi.
Akizungumzia
ahadi ya balozi Sefue kupangiwa kazi nyingine, Mhadhiri wa Chuo cha
Diplomasia, Dk Ahmed Kiwanuka alisema kauli hiyo ni ya kawaida na
humaanisha dhamira ya kweli ya Rais kutafuta nafasi mpya ya kumpeleka
mhusika hata kama itachukua muda mrefu. “Kuna kazi nyingine kama za
ubalozi ni lazima zipitie mchakato mrefu siyo rahisi kama watu
wanavyofikiri. Hivyo Rais hawezi ghafla akasema ‘namteua fulani kuwa
balozi wa nchi fulani’ kama jina la huyo mtu halijakubaliwa upande wa
pili,” alisema Dk Kiwanuka.
|
||
Posted: 08 Mar 2016 01:58 AM PST
Ukaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni za fedha za serikali za mitaa (LAFM) ya mwaka 2009 na (LAAM) ya mwaka 2009 na kanuni za ununuzi za mwaka 2013, sambamba na maelekezo ya kamati ya fedha. Kwa mujibu wa taarifa za ukaguzi huo ambao Raia Mwema imeona nakala yake, fedha zilizopotea ni zaidi ya milioni 500, kati ya mwezi Julai 2014 na Juni 2015, ikiwa ni miezi minne kabla ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba, mwaka jana. Hali hiyo inatokana kinachoelezwa kuwa ni udhaifu mkubwa wa wakala wa kukusanya mapato ya halmashauri ambaye ni kampuni maarufu ya Max-Malipo inayojishughulisha na biashara fedha kwa njia ya mtandao. Kampuni hiyo ya Max-Malipo iliingia mkataba unaodaiwa kuwa na utata mkubwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha Julai mwaka jana, kwa shinikizo kubwa la Mkurugenzi wa Jiji, Idd Juma, pamoja na baadhi ya madiwani wakiwamo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa wakati huo. Mapato yalivyopotea Taarifa hiyo inaonyesha kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu, imegundulika kuwa mapato yanayokusanywa na mashine za maxcom yalishuka badala ya kuongezeka. “Wakati wa ukaguzi na ukusanyaji wa mapato kwa vyanzo vinavyokusanywa na mashine za maxcom, masoko, vituo vya mabasi, vyoo na machinjio mapato yamepungua kwa asilimia 40 tofauti na kipindi cha awali makusanyo yalipokuwa yanafanywa na mawakala,” inasomeka sehemu ya taarifa ya ukaguzi huo. Inaendelea zaidi: “Mapato yanashuka kutokana na wakusanya mapato kutotoa stakabadhi za mashine kwa wateja na kusababisha makato hayo yasiyokatiwa stakabadhi kutoingia halmashauri, kinyume cha kanuni za fedha za serikali za mitaa”. Pamoja na taarifa hiyo ya ukaguzi, habari kutoka ndani ya Jiji zinadai kuwa halmashauri imeingia hasara kubwa ya kupoteza mapato yake kutokana na mfumo huo na mkataba ambao unadaiwa kuwa umejaa utapeli. Akitoa mfano wa hasara hiyo, mmoja wa watumishi wa halmashauri aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alieleza kuwa kabla ya kuingia mkataba na Max-Malipo wakala aliyekuwa akisimamia choo cha Soko la Kilombero alikuwa anawasilisha kiasi cha shilingi milioni 1.5 kwa mwezi. “Kwa Max-Malipo mapato yameshuka na pia halmashauri inalazimika kulipa gharama za uendeshaji kama maji na umeme kila mwezi kati ya shilingi 500,000 na 800,000 pamoja na mshahara wa msimamizi, hivyo kukosa mapato kwa asilimia 50,” alidai mtoa taarifa huyo. Takwimu za ukaguzi zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ya Machi ,Aprili na Mei mwaka 2015 kabla ya kuingia mkataba na Max-Malipo Halmashauri ya Jiji la Arusha ilikuwa inakusanya wastani wa shilingi 95,225,018 kwa mwezi. Fedha hizo ni kutoka vyanzo vya mapato vya vituo vyote vya mabasi, vyoo vya umma, machinjio na masoko yote ya Jiji. Taarifa hiyo inabainisha kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu kampuni ya Max-Malipo ilikusanya wastani wa shilingi 56,768,104 na 83,296072, hivyo halmashauri kupoteza zaidi ya shilingi milioni 100. Ufisadi Arusha Meat Aidha ufisadi mkubwa umebainika katika ukaguzi huo, katika kampuni tanzu ya Arusha Meat inayomilikiwa na Jiji ambayo inasimamia machinjio ya Jiji na kiwanda cha kusindika nyama cha Arusha Meat. Ukaguzi huo unaonyesha kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni za matumizi ya fedha za serikali kutokana na usimamizi mbovu wa Mkurugenzi wa Jiji, mweka hazina na watumishi wa kiwanda hicho. Miongoni mwa mfano wa matumizi mabaya ya kanuni za fedha ni kukosekana kwa hati za malipo (Invoice) yenye thamani ya shilingi 178,164,308 kati ya Julai 2014 na Juni 2015. Ukaguzi unaonyeha kuwa katika kipindi hicho malipo yenye thamani ya shilingi 64,604,574 pia yalikosa uthibitisho na viambatanisho halali kinyume cha sheria namba 10 ya kifungu cha 2 (d) cha mwaka 2010, kinachohusiana na usimamizi wa fedha za serikali za mitaa. Pia ilibainika kuwa fedha za mauzo ya duka la nyama la kampuni hiyo lililopo eneo la Nanenane katika Jiji la Arusha kiasi cha shilingi 9,614,000 hazikuwasilishwa benki kinyume cha sheria ya fedha za serikali za mitaa ya mwaka 2010, namba 37 kifungu cha tatu. Mkaguzi huyo anafafanua kuwa hatua ya kutopelekwa kwa fedha hizo benki kumesababisha kampuni hiyo kukosa uwazi na kuzua upotevu wa fedha za umma. Ukaguzi huo umeendelea kubainisha kuwa kampuni hiyo ya nyama pia imepoteza kiasi cha shilingi 16,635,320 kati ya Julai 2014 na Juni 2015, kabla ya kuwasilishwa benki na hakukuwa na vielelezo vyovyote vya matumizi ya fedha hizo. Aidha pia imebainika kuwa kati ya siku 4 hadi 54 daktari msimamizi wa ukaguzi wa nyama katika kiwanda hicho hakuwasilisha benki malipo ya shilingi milioni 15,770,000, kinyume cha sheria ya fedha za serikali za mitaa namba tano na 50 ya mwaka 2009. Katika idara nyingine za halmashauri, ukaguzi unaonyesha kuwa katika kipindi cha Julai 2015 na Septemba 2015 kiasi cha shilingi 12,280,750 zimelipwa kwa wadai mbalimbali (creditors) ambao hawako katika orodha ya wadai wa Jiji. Taarifa hiyo inaendelea: “Pia hati za malipo zenye thamani ya shilingi 339,044,587,22 katika idara mbalimbali za halmashauri zilikosekana kati ya Julai 2015 na Septemba 2015” Pia watumishi 49 wa Jiji walishindwa kurejesha masurufu wala kuingizwa katika rejista yenye thamani ya shilingi 144,777,100.45, wakiwamo maofisa wa ngazi za juu katika |
No comments:
Post a Comment