Naibu
katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Warsha
kwa maafisa wa mipakani kuhusu usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo
na Bioteknolojia ya kisasa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Julius Ningu na kushoto ni Afisa Mazingira
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Esta Makwaia. Warsha hii imefanyika leo
kwenye Hotel ya La kairo jijini Mwanza
Washiriki
wa Warsha ya Usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia
ya kisasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi (katikati) Mara
baada ya kufungua warsha hiyo kwenye Hoteli ya La kairo Jiji Mwanza
…………………………………………….
Lulu Mussa na Ali Meja
Mwanza
Imeelezwa kuwa Tanzania kama nchi
nyingine haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia kutokana na
utandawazi na maendeleo duniani kote, kwa kuwa bioteknolojia ya kisasa
ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini, kuboresha
kilimo, uzalishaji viwandani, afya na hifadhi ya mazingira.
Hayo yamesemwa leo na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava katika warsha ya
siku moja kwa maafisa wa mipakani kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, warsha
iliyolenga kukuza uelewa kwa watendaji wanaosimamia mazao na bidhaa
zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa.
Amesema, Serikali kwa kutambua
mchango mkubwa unaoweza kupatikana kutokana na matumizi ya bioteknolojia
ya kisasa katika sekta za afya, kilimo, viwanda na mazingira, imeridhia
Itifaki ya Cartagena ya Mkataba wa Bioanuai mwaka 2003 kwa lengo la
kuhifadhi mazingira kwa kuzingatia usalama katika usafirishaji, kuunda
na kupitisha mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa matumizi salama ya
Bioteknolojia mwaka 2007.
Eng. Mwihava amewaasa watendaji
katika maeneo ya mipakani kuwa na usimamizi madhubuti katika maeneo yao
ya kazi kwa kuwa mipaka kati ya Tanzania na nchi nyingine ndiyo njia kuu
za uingizaji wa mazao na bidhaa zitokazo nje.
Pamoja na faida za bioteknolojia
hiyo ya kisasa Eng. Mwihava amewataka watendaji hao kuwa makini na
athari zinazoweza kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo pale
itakapotumiwa bila kufuata taratibu za usalama zilizowekwa.
Warsha hii ya siku moja kwa
imewashirikisha maafisa forodha, Maafisa Afya na watafiti wa Mazao
kutoka Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera, kutoka Idara , wakala za
Serikali na sekta binafsi.
No comments:
Post a Comment