Mkurgenzi
wa Tanpress Mobini Sarya akiwa kwenye usafiri wa pikipiki akitoka
kwenye visiwa vya Nyamango na Chembaya eneo la Mwalo wa Kanyara ziwa
Victoria mkoani Mwanza ambako alikwenda kuchunguza upatikanaji wa
huduma za afya katika visiwa hivyo Novemba mwaka huu.
Hii ndiyo ofisi ya kijiji cha Lushamba inayohudumia visiwa saba vyenye wakazi elfu 25 .
Hii
ndiyo ofisi ya kitongoji cha Kanyara kwa juu kama inavyoonekana kwa
chini ni Sero (Mahabusu)inayotumika kuwahifadhi wa halifu ambayo
mwandishi wa habari Mobini Sarya aliwekwa chini ya ulinzi kwa masaa 6.
Wakazi wa kisiwa cha Nyamango na Soswa wakigombania usafiri wa boti kwa ajili ya kuelekea Sengerema mkoani Mwanza.
……………………………………………………………
Nyamango/Soswa visiwa vyenye fursa tele za uwekezaji
zinahitajika zahanati,shule na kumbi za starehe.
Na Tanpress,Nyamango
NYAMANGO na Chembaya ni visiwa
viliopo maili 46 Mgharibi mwa jijini Mwanza ingawa vinahesabiwa kuwa
vipo wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.
Hivi visiwa vina undwa na
vitongoji viwili vyenye visiwa vinne vikijulikana kwa majina ya
kitongoji cha Nyamango/Chamagati na Chembaya/soswa vikiwa maeneo ya
karibu.
Vinakisiwa kuwa na wakazi zaidi ya
10,000 ambao wanategemea shughuli za uvuvi wa dagaa na samaki
wanaopatikana katika ziwa viktoria.
Usafiri unaotumika kwenda kwenye
visiwa hivyo ni boti au meli za watu binafsi,ambazo hutumia masaa 12
kutoka jijini mwanza eneo hilo na mara nyingi boti ya mwendo kasi
huingia saa mbili usiku.
Aidha kutoka katika visiwa hivi
hadi kwenye mwalo wa Kanyara ambayo ni nchi kavu ya wilaya ya Sengerema
boti hutumia masaa manne hadi masaa matatu kufika nchi kavu.
Pia kutoka eneo la kitongoji cha Kanyara usafiri ni wa shida Km.80 hadi kufika Sengerema mjini zilipo huduma zote za kijamii.
Eneo hilo lina vitongoji viwili
vinavyoundwa na visiwa vine ambavyo ni Soswa/Chembaya na
Nyamango/Chamagati ni katika eneo hilo lenye makazi ya kudumu ya watu
ndipo frusa za uwekezaji zipojitokeza.
Hivi karibuni Mwandishi wa Shirika
la habari Tanpress alifika kwenye visiwa hivyo kwa lengo la kukusanya
habari na matukio ndipo alipojionea frusa nyingi za uwekezaji.
Kwanza licha ya kwamba wavuvi
wengi ni watu wanaopenda starehe hasa za ulevi lakini ‘viwanja
vyakujirusha’kuburudika ni kama havitoshi.
Maeneo mbalimbali ambayo mwandishi
wa Tanpress alitembelea alikuta wenyeji wakipata vinywaji kwenye baa
zinazofanana na vilabu vya Pombe za kienyeji jambo linaloonyesha kuwa
maeneo hayo yanahitajika uwekezaji wa baa na mahoteli ya kisasa.
Aidha nishati ya umeme kwenye eneo
hilo inahitajika kwa haraka kwani wengi wanatumia jeneretor ambazo
hawamudu kununua mafuta hivyo hata wale wachache waliojitolea kujenga
nyumba za kulala wageni wanawasha vibatari wasijue la kufanya.
Hivyo anahitajika ,mwekezaji
mkubwa aweke mashine inayotumia mafuta ya diseli kwa ajili ya kuzalisha
umeme wa kutosha katika eneo hilo,ambalo kwasasa lipo gizani ingawa
wenyeji wanahitaji huduma hiyo.
Pia sio lazima itumike mashine ya
mafuta pia hata umeme wa jua au kufuka mitambo ya upepo kwasababu maeneo
yale hakuna miti ya kuzuia upepo huo.
Baadhi ya maeneo ,mengine au hata
visiwa vingine mashine za kufua umeme kwa kutumia mafuta ya diseli ndio
zinatumika kusambaza umeme jambo ambalo halijafanyika kwenye visiwa vya
Nyamango.
Frusa nyingine uwekeza ambayo
inalipa ni kituo cha afya au zahanati,licha ya kwamba wavuvi
wanafamilia zinazohitaji huduma ya afya wanapo ugua au akinamama
wanapotaka kujifungua huduma hiyo haipo kabisa kwenye visiwa hivyo.
Kwa hiyo akitokea mwekezaji
akafungua zahanati yenye uwezo wa kuzalisha akinamama wajawazito anaweza
akanufaika kwa haraka kwasababu inavyoonekana serikali imeamua
kutelekeza wakazi hao na haina mpango wowote wa kuwajengea zahanati.
Kwasasa zahanati sio jambo la
mjadala inahitajika kwa haraka kuweza kuokoa maisha ya akinamama
wajawazito na watu wa kawaida wanao umia kwenye starehe zikiwemo ulevi.
Ni vyema kama mwekezaji anavutiwa
na uwekezaji huo akajenga kabisa kituo kikubwa cha afya kwasababu hakuna
kituo karibu hata kwenye visiwa vya jirani kama zilagula na Yozwa bado
huduma hiyo wana kwenda kuitafuta mbali.
Elimu ni frusa nyingine ya
uwekezaji inayohitaji watu wenye mitaji kwani pamoja na kwamba wavuvi
hao wanafamilia zao eneo hilo lakini kuna shule moja ya umma ambayo hata
hivyo haitoshi mahitaji.
Shule hiyo ya msingi inajulikana
kama Soswa shule ya Msingi bado haijaweza kutoa elimu bora kutokana na
kukosekana kwa walimu wa kutosha eneo la visiwa hivyo.
Kwa hiyo zinahitajika shule za
awali kwa kila kisiwa ambapo kuna visiwa vinne pia zinatakiwa shule
binafsi za sekondari na msingi au hata vyuo vya michezo ya majini kwa
ajili ya wagoeleaji.
Frusa zingine niliziona ni kuweka
boti za mwendo kasi kwa ajili ya kuwakimbiza wagonjwa hospitalini na
kuanzisha kampuni za ulinzi kwani hivi sasa baada ya uvamizi kuwepo,
wakazi wa pale wameanza kukodi walinzi kutoka Mwanza ambapo ni mbali
zaidi.
Zipo frusa nyingi za uwekezaji
hata kwenye soko la chakula cha kuku na wanyama wengine lakini kama wewe
ni mwekezaji unaweza kufika huko ukajionea mwenyewe.
www.mobinday.blogsopot.com 0753399 579 mobinsons@yahoo.com
No comments:
Post a Comment