Hoteli ya kitalii ya Lakairo Hotel ya jijini Mwanza,imejitokeza kudhamini shindano la Miss Utalii Vyuo Vikuu - Kanda ya kati,lililopangwa kufanyika Dodoma siku ya uhuru tarehe 9-12-2011.
Akithibitisha udhamini huo, mkurugenzi wa hoteli hiyo inayomilkiwa na Mheshimiwa Lameck Okambo Airo mbunge wa wa jimbo la Rorya,Daniel Airo alisema kuwa hoteli hiyo inatoa jumla ya shilingi lakitano (500,000/=) kwa ajili ya kuchangia zawadi za washindi wa shindano hilo,linaloshirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mikoa ya kanda ya kati,ikiwemo mikoa ya Dodoma,Singida na Tabora. Daniel alisema kuwa wameamua kudhamini shindano hilo kwa kutambua umuhimu na mchango wake katika kukuza sekta ya utalii nchini,aliongeza kuwa ushiriki wa wanafunzi wa vyuo vikuu katika shindano hilo ni fulsa nyingine ya pekee ya kukuza utalii wa ndani ,kwani iwapo wasomi hao wakihamasika na suala zima la utalii hususani utalii wa ndani basi ni rahisi jamii kuiga na kufuata mfano wa wasomi hao,ambao pia ndio viongozi watarajiwa katika nyanja mbalimbali nchini baada ya kuhitimu masomo yao.
Wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini shindano hilo ni Duka la mavazi na vipodozi la Happy Fashion wanaotoa zawadi yenye thamani ya shilingi laki tatu (300,000/),Master Pub , NAM Hotel,Becko Qulity Centre wanatoa zawadi yenye thamani ya laki tatu kwa mshindi wa vipaji,New Soft Saloon,CF Communication & Stationary, Club 84 na Royal Village Hotel,PAPA MSOFE.
Washindi wa 1-5 na wa taji la vipaji watawakilisha Vyuo vikuu kanda ya kati katika fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2011/12 zilizopangwa kufanyika mwezi February 2012, ambapo washindi wa taifa watawakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya Miss Tourism World,Miss United Nations,Miss Tourism United Nations,Miss Heritage World,Miss Globe International,Miss Tourism University World na United World International Pageant
No comments:
Post a Comment