Wazee wakiwa kwenye kongamano la
wazee kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mpanda kujadili
changamoto zinazowakabili wakati wa kupatiwa matibabu.
Na Kibada Kibada-Katavi.
Wahudumu wa Afya wameendelea
kuwanyanyapaa wazee wawapo hospitalini kupata huduma ya Afya kwa
kuwaacha wakae asubuhi hadi jioni ,huku wenyewe wakifanya kazi zao
nyingine.
Pia wakitibiwa na Daktari mara
nyingi huambiwa wakatafute dawa madukani hata kama zipo hospitalini na
ukiuliza kwa nini hujibu hawahitaji usumbufu.
Hayo yameelezwa na Katibu wa
Shirika la Wazee saidia lenye makao yake Wilayani Kasulu Mkoani
Cotlida Kokupima wakati akiwasilisha salamu za wazee kutoka Mkoani
kigoma kwenye kongamano la wazee lililofanyika Mjini Mpanda Mkoa wa
Katavi.
Bibi Kokupima ameeleza
changamoto zinazowakabiliwa wazee katika maeneo mbalimbali zikiwemo na
manyanyaso hayo wanayofanyiwa wazee wakiwa katika Zahanati,Vituo vya
Afya Pamoja na Kwenye Hospitali mbalimbali hapa nchini.
Changamoto hizo ni kuwa wakienda
kutibiwa na wakishaandikiwa dawa wanaambiwa hazipo waende wakanunue
madukani wakati mwingine wanakuwa hawana hela matokeo yake wanarudi
nyumbani kulala bila kupata dawa na mwisho ni kufa.
Changamoto ya usafiri kutoka
nyumba hadi kufika kwenye huduma za jamii hasa matibabu kwa wazee wenye
umri mkubwa ni taabu,hawana uwezo wa kuzifuata dawa dukani hata kama
watakuwa na fedha.
Kwa Upande wake mwakilishi wa
shirika la Afya la Wazee Duniani Athman Daniel ameeleza kuwa shirika
lake kwa kusaidiana na wadau mbalimbali na wazee limeweza kuchangia
kuisukuma serikali kuona uwezekano wa kuwapatia wazee malipo ya uzeeni
na mchakato unaenda vizuri na wakati wowote suala hilo litafanikiwa.
Akizungumzia Halmashauri ya
Mpanda amesifu juhudi zilizofanywa katika kuwahudumia wazee kwa kutenga
chumba cha kiliniki ya wazee na wanapatiwa huduma hapo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI KUPITISHA SHERIA YAO.
No comments:
Post a Comment