WANACHAMA 75 kutoka Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Msasani Jimbo la Kawe akiwemo
Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake Chadema Kawe (BAWACHA) wamejiunga
na chama cha Alliance for Change and Transparent (ATC-Tanzania).
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti
wa ACT-Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam Khamis Chambuso wakati
akiwakabidhi kadi za chama hicho leo jijini Dar es Salaam.
Chambuso alisema wanachama hao
pamoja na wanachama wengine kutoKA Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CHAUMA
wamejiunga na ACT- Tanzania kwa mapenzi yao bila kushawishi na kitu
chochote.
Alisema kwa siku jana wamepokea
wanachama 78 ambapo mmoja anatokea mkoa wa Kigoma na wengine wanatokea
mkoa wa Dar es Salaam wengi wao wakiwa ni kutoka CHADEMA.
“Kimsingi tunajisikia faraja
kuona Watanzania waliowengi wanaanza kutambua umuhimu wetu na wameamua
kujiunga na ACT- Tanzania hivyo wanatuongeza nguvu ya kufanya mabadiliko
ya nchi”, alisema.
Alisema ACT-Tanzania kina
dhamira yua kweli ya kuhakikisha kuwa mfumo mzima wa nchi unabadilika
ikiwa nin pamoja na kushirikisha jamii ya Watanzania inafaidika na
rasilimali zilizopo hapa nchini.
Chambuso alisema ACT- Tanzania
haijaja kwa ajili ya kubomoa vyama vingine ila misingi yake ndio chanzo
cha watu kutoka vyama mbalimbali kuhitaji kujiunga nao.
Mwenyekiti huyo aliwataka
wachama hao wapya kuhakikisha kuwa ni sehemu ya mafanikio ya
ACT-Tanzania kwa kuongeza wanachama zaidi.
Kwa upande wake Mhandisi
Mohammed Ngulangwa ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa siku
nyingi tangu mwaka 1997 alisema kilichomuondoa CCM ni chama hicho
kushindwa kutekeza sera zake.
Ngulagwa ambaye mwaka 2010
aliingia katika kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge ndani ya chama Jimbo
la Temeke alisema kimsingi chama cha ACT-Tanzania ndicho chenye misingi
sahihi ya kidemokrasia.
Alisema juhudi zake katika siasa
atazionyesha kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa chama hicho kipya
kinafanya vizuri katika medani za siasa hapa nchini.
No comments:
Post a Comment