Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo akizungumza katika uzinduzi huo.
Mtaalamu wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Meneja
Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akizungumza katika uzinduzi huo. Kampuni
ya Tigo, Nokia na Microsoft ndio wadau mpango huo.
Meneja Mawasiliano wa Microsoft Mobile Devices, Lilian Nganda akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia Dk.Hassan Mshinda akizungumza katika
uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi huo.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, John Mgodo
(katikati), akiangalia simu wakati akiwaelekeza namna ya kutumia simu
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania, Peter Riima (kushoto) na
Mrashani Katebeleza, wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha
wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na
vifaa vingine vya kielektroniki Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Mkuu
wa Tigo, Diego Gutierrez.
Hapa uzinduzi huo ukifanyika.
‘ Ni kama anasema’ Niacheni nipo kazini nachukua tukio hili nikawahabarishe wengine, chezea mimi nyiee
Wadau mbalimbali na wanahabari wakiwa kwenye
hafla hiyo ya uzinduzi.
Wadau na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Dotto Mwaibale
WANAFUNZI
nchini wametakiwa kutumia mitandao hasa ya simu za mikononi kwa ajili
ya kujifunzia masomo mbalimbali badala ya kutumia katika matumizi
yasiofaa.
Mwito
huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na
Teknolojia, John Mgodo wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwawezesha
wanafunzi kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mkononi na
vifaa vingine vya kielektroniki uliofanyika Dar es Salaam leo.
Alisema
progamu hiyo imefika wakati muafaka na itawasaidia wanafunzi kujifunza
somo hilo muhimu katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Alisema
programu hiyo imeletwa nchini na Kampuni ya Nokia, Tigo kwa
kushirikiana na Microsoft, ambapo serikali kupitia Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (Costech) inasimamia kwa karibu mpango huo.
Alisema
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika programu hiyo imesaidia
kupata mahudhui ya kihisabati jambo litakalo wasaidia wanafunzi kuwa
makini kitaaluma.
Alisema
matumizi hayo ya simu katika kujifunza hisabati yatakuwa yakifanyika
katika muda wa ziada baada ya masomo kwa vile licha ya wanafunzi
kumiliki simu lakini hawaruhusiwi kuwa nazo mashuleni.
Mgodo alisema mpango huo kwa sasa upo katika majaribio ukifanikiwa wanaweza kuuingiza katika mitaala ya taifa.
Mtaalamu
wa mradi huo kutoka Kampuni ya Nokia, Riita Vanska alisema mpango huo
umekuwa ukiongeza weredi kwa wanafunzi katika somo la hisabati na ni
muhimu katika kipindi hiki cha maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dk.Hassan Mshinda
alisema tume hiyo ilifanyamchakato na kuukubali mpango huo ambao ni
muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaupungufu mkubwa wa
wataalamu wa sayansi wanaotokana na kufaulu kwa somo la hisabati.
“Mradi huu tuliona unafaa kwani utasaidia kuongeza wanasayansi hivyo tuliupokea kwa mikono miwili” alisema Dk.Mshinda.
No comments:
Post a Comment