Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa BAWACHA taifa.
……………………………………………………………..
Kipimo Abdallah
ALIYEKUWA Katibu Mwenezi wa
Baraza la Wanawake Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Jimbo la
Kawe, Batuli Kivuma ambaye amejiunga na chama cha Alliance for Change
and Transparent (ACT-Tanzania amesema kilichomuondoa CHADEMA ni ukabila
ulioota mizizi kwa muda mrefu.
Kivuma ambaye awali alikuwa
mwanachama wa Chama Cha Wananchi CUF alisema aliamini kuwa chama hicho
kinasimamia demokrasia jambo ambalo limeshindikana hasa ukiwa hotekei
mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema tangu ajiunge katika
chama hicho amekuwa na juhudi za kukijenga chama hasa Kata ya Msasani na
jimbo zima la Kawe ila juhudi zake zimekuwa zikikwamishwa kwa misingi
ya ukabila.
Katibu Mwenezi huyo wa zamani wa
BAWACHA alisema katika kudhihirisha hilo alishiriki kwenye mchakato wa
kugombea nafasi ya Udiwani viti maalum mwaka 2010 ambapo alishinda ila
aliondolewa kwa kigezo cha yeye ni Mdigo na wakapewa nafasi hiyo
Wachaga.
“Kusema ukweli suala la kuhama
vyama sio zuri ila inafikia mahali unashindwa kuvumilia kwani nimekuwa
nikionewa mara kwa mara katika chaguzi na ukiangalia vizuri msingi wake
ni ukabilia ambao unawabeba Wachaga” , alisema.
Kivuma alisema alikuwa
akikipenda sana chama hicho lakini ubaguzi uliopo amefikia mwisho wa
uvumilivu na kwamba anahitaji kuonyesha jitihada zake kwingine.
Alisema suala hilo la ukabila
lilikidhiri katika uchaguzi mkuu ambao ulifanyika hivi karibuni hasa
katika upande wa BAWACHA ambapo juhudi zilifanywa kuanzia ngazi ya chini
hadi Taifa.
Mwenezi huyo wa zamani wa
BAWACHA alisema hata upatikanaji wa Mwenyekiti wa BAWACHA wa sasa Halima
Mdee ulitawaliwa na ukabila ikiwa ni agizo la Mwenyekiti Taifa Freeman
Mbowe.
“Unajua hili neno demokrasia
wanalielewa je bwana kwani kwa ufahamu wangu ni kuhakikisha kuwa jamii
inaacha pale inapofanya maamuzi yake ila huku ni kinyume”, aliongezea
Kivuma.
Kivuma alisema atahakikisha kuwa anakibomoa CHADEMA hasa katika Jimbo la Kawe ambapo amefanya kazi za kisiasa kwa muda mrefu.
Kwa upande wake aliyekuwa Mjumbe
wa Mtaa Serikali ya Mtaa wa Matofalini Ujiji Kigoma Yassin Mohamed
alisema ni vema vyama vikatambua kuwa hakuna uadui baina yao na kuhama
chama ni haki ya mtu.
Alitolea mfano hali ya kisiasa
ilivyokuwa siku za nyuma kati ya chama na CHADEMA na CUF hali ambayo kwa
sasa haipo na vinafanya kazi pamoja.
Mohamed alisema ameamua kujiunga na ACT-Tanzania na kuondoka CHADEMA ili kupata uhuru wa kupigania demokrasia ya kweli.
No comments:
Post a Comment