Mawaziri
wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya
wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi
hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya
biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mkataba huo
umesainiwa jijini Dar es Salaam leo na Waziri wa Nishati na Madini
Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Waziri wa Wizara ya
Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia , Christopher Yaruma
(kushoto) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya , Davis Chirchir (kulia)
. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Migodi ,
Nishati na Maendeleo ya Maji Zambia, Charity Mwansa, Katibu Mkuu Wizara
ya Nishati na Madini , Tanzania , Eliakim Maswi na Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Petroli Kenya, Mhandisi Joseph Njoroge.
Mawaziri
wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya ,
Waziri wa Wizara ya Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia ,
Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini , Profesa
Sospeter Muhongo Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli
Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano
kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja
ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada
baina ya nchi hizo mara baada ya kusaini.
Mawaziri
wa wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya ,
Waziri wa Wizara ya Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia ,
Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli
Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara
baada ya kusaini.
Sehemu
wa wadau walihudhuria hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha
dhamira ya Serikali ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya kujenga
miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya
kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mbali na Wataalamu kutoka
katika nchi hizo, hafla hiyo imehudhuriwa uwakilishi wa COMESA,
Mashirika ya Umeme kutoka nchi hizo na baadhi ya washirika wa Maendeleo
wakiwemo Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Norway, Shirika la
Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank (AfDB), Ubalozi wa
Ufaransa.
Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Nchi za Zambia, Tanzania na Kenya zimesaini Mkataba wa Makubaliano
kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja
ya kusafirisha umeme (ZTK) na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa
ziada baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani Afrika. Akiongea katika
hafla hiyo Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania Profesa Sospeter
Muhongo ameeleza kuwa, mradi huo wa pamoja unalenga kuondoa tatizo la
upungufu wa nishati ya umeme baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani
Afrika jambo ambalo litachangia katika kukuza uchumi wa mataifa hayo.
Naye, Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia ,
Christopher Yaruma ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo sio tu
utaziwezesha nchi hizo kufanya biashara bali pia utafungua fursa za
uwekezaji na kusaidia katika kuondoa umaskini miongoni mwa nchi
wanachama kutokana kuzitumia fursa mbalimbali zinazotokana na nishati ya
umeme. Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis
Chirchir amewataka washirika wa maendeleo kusaidia katika kuwezesha
utekelezaji wa mradi huo wa kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha
umeme baina ya nchi hizo kutokana na manufaa yake kwa bara la Afrika na
kuongeza kuwa, kutokana na uwepo wa rasilimali asilia za kutosha katika
nchi hizo hakuna sababu ya kuwepo tatizo la nishati katika nchi hizo na
barani Afrika. Naye, Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Soko la pamoja
la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi
(COMESA), Dkt. Kipyego Cheluget amezipongeza nchi hizo kwa kuuendeleza
utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua kipindi kirefu na kuueleza
kuwa, ni miongoni mwa miradi 16 ya kipaumbele na kimaendeleo kwa Afrika.
Aidha, kwa upande wao Washirika wa maendeleo waliohudhuria hafla hiyo,
wameonesha kufurahishwa kwao na dhamira ya nchi hizo na kuahidi
kushirikana na nchi hizo kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. Miongoni
mwa washirika wa maendeleo waliohudhuria ni pamoja na uwakilishi wa
Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo
la Japani (JICA), African Development Bank(AfDB) na Ubalozi wa Ufaransa.
No comments:
Post a Comment