Kaimu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akizungumza na wajumbe
muda mchache kabla ya Mgeni rasmi kufungua kikao rasmi. Kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dedengo na kulia Chama cha Watoa Huduma
binafsi za Afya Nchini, Dr. Samweli Ogillo.
SERIKALI imetoa rai kwa wananchi
kutoa taarifa kwa mgonjwa yeyote mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebora ili
aweze kupati msaada wa kitabibu hali ambayo itapunguza maambuzi kwa watu
wengi .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa
Wilya ya Tanga wakati akifungua kikao cha maelekezo huhusu ugonjwa
hatari wa Ebola na dhana ya ushirikiano baina ya Sekta binafsi na Sekta
ya Umma kwa madaktari na wauguzi kutoka serikalini na sekta binafsi
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Rodasaksa Hospiali ya Mkoa wa Tanga
(Bombo).
Kikao hicho ni moja ya jitihada
ambazo zinachukuliwa na Mkoa wa Tanga katika kutoa uelewa wa ugonjwa
huo hatari ambao sasa umekuwa tishio katika baadhi ya maeneo ya Afrika.
Vile vile ametoa wito kwa sekta ya umma na sekta binafsi kuweka nguvu
zao pamoja katika kuhakikisha wanachi wanapata huduma bora za afya.
Akielezea mkakati wa Mkoa dhidi ya
jinsi gani Mkoa umejiandaa endapo atapatikana mgonjwa wa Ebola katika
Mkoa wa Tanga, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr Asha Mahita
amesema kuwa tayari maeneo mbalimbali yenye vifaa maalumu yametengwa ili
kutoa huduma ya kitabibu kwa wagonjwa wa aina hiyo. Maeneo hayo ni
pamoja na eneo la Masiwani lilipo jengo la Hospitali ya Wilaya ya Tanga
na kituo kingine kipo Mpakani Horohoro.
Serikali pia imekuchukua tahadhali
katika maeneo ya mpakani hasa eneo la Horohoro mpaka wa Tanzania na
Kenye na uwanja wa ndege kwa kuweka kifaa maalumu cha kuweza kupima na
kutambua msafiri mwenye maambukizi ya Ugonjwa wa Ebola. Hatua ambayo
imefikiwa baada ya kusikia kuwepo mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za
jirani na hasa Afrika.
Akifafanua dhana ya ushirikiano
kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kutoa huduma za afya,
Dr.Samweli Ogillo ambaye ni Mtendaji Mkuu kutoka chama cha Watoa huduma
Binafsi Nchini ( APHFTA)amesema ni jambo la msingi iwapo Serikali na
Sekta binafsi zitaweka nguvu ya pamoja ili kudhibiti na kuzuia ebola
kuingia nchini kwa sababu upande mmoja peke yake hauwezi.
Hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote
mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebola ambaye ameripotiwa kupatikana katika
nchi ya Tanzania. Historia inaonyesha mwaka 2012 Mwezi wa Julai
ulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Uganda eneo linaitwa
Kabaale ambapo zaidi ya watu 14 walipoteza maisha.
Ebola ni ugonjwa hatari
unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “Ebola
Virusi na husambaa kwa haraka sana . Dalili zake ni pamoja na homa kali
inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua,
njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, machoni kutapika na kuharisha
damu. Stori & Picha na Monica Laurent, Afisa Habari Tanga
No comments:
Post a Comment