Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Simba kabla ya mpambano wa Fainali
ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Mtibwa Sugar katika kusherehekea miaka
51 ya Mapinduzi ya Zanzibar mchezo uliofanyika jana Uwanja wa Amaan
Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Wananchi
na Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia kwa makini mchezo wa fainali
ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana
katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika
kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo simba
iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3, [Picha na
Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Simba Hassan Izhaka baada ya
kuifunga Mtibwa kwa matuta 4-3 mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi
uliofanyika jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya
Zanzibar katika uwanja wa Amaan Studium,[Picha na Ikulu.]
Wachezaji
wa Timu ya Simba wakisherehekea ushindi wao baada ya kuwafunga kwa
matuta timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa fainali ya
kombe la Mapinduzi 4-3 katika uwanja wa Amaan studium Mjini Unguja jana
katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na
Ikulu.]
Mashabiki
wa Timu ya Simba Wengundu wa Msimbazi walipokuwa katika jukwa la Saa
katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja wakishangilia timu yao
ilipocheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika fainali ya kombe la
Mapinduzi,Timu hiyo ya Simba ilishinda kwa matuta 4-3ikiwa ni
kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na
Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk
(kushoto) wakiangalia mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati
ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan Studium
Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar ambapo simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa
matuta 4-3 , [Picha na Ikulu.]
No comments:
Post a Comment