Ayubu
Lihunga Mkurugenzi wa Shirika la Vijana wajasiriamali na Uwezeshaji
Tanzania (TYEEO) akizungumza na wajasiriamali wakati alipokuwa
akimkaribisha mgeni rasmi kwenye sherehe ya uzinduzi wa taasisi hiyo
niliyofanyika kwenye viwanja vya maonyesha vya Sabasaba jijini Dar es
salaam leo, Katikati ni Sadiki Kusiama Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha
Sayansi na Teknolojia Mbeya.
Sadiki
Kusiama Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya
akihijiwa na waandishi wa habari wakati wa sherehe ya uzinduzi wa taasisi hiyo VICOBA iliyofanyika kwenye viwanja vya maonyesho Sabasaba jijini Dar es salaam
Baadhi ya wana VICOBA wajasiriamali wakiwa katika sherehe hiyo
Baadhi ya wana VICOBA wajasiriamali wakiwa katika sherehe hiyo
………………………………………………………………………………………………
VIJANA wameshauriwa kuungana
pamoja na kuweza kutumia rasilimali zilizopo hapa nchini kwa lengo la
kujiendeleza na kujitoa katika lindi la umasikini.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es
Salaam leo katika uzinduzi wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya TEEYO
na Mhadhiri msaidizi wa Chuo kikuu cha sayansi na Teknolojia Mbeya
Sadiki kusiama.
kusiama alisema kuwa hakuna njia
nyingine kwa vijana ya kuweza kuyafikia maendeleo kama si kujiunga
katika vikundi ili kuweza kupata fursa zinzojitokeza katika jamii.
“Binafsi nimefarijika kwa hatua
hii ambayo taasisi hii ya TEEYO ilichokifanya katika jamii ni dhahiri
kuwa vijana wengi wataweza kupata fursa na mwisho wasiku kuweza
kujinasua katika umasikini hivyo watanzania wanapaswa kuchangia jitihada
hizi,”alisema Sadick
Alisema kuwa kupitia taasisi kama
hizo ambazo zinafanya kazi kubwa kwa ajili ya kuwanasua watanzania
kuondoka katika umasikini serikakali ingeweka mazingira mazuri na hasa
katika kupunguza bei ya vifaa vya ujenziu vinavyo zalishwa hapa nchini
ili kutoa fursa kwa wajasiliamali kuweza kuwa na nyumba za kisasa.
Pia Sadick aliipongeza taasisi
hiyo kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ikiwemo kuunga juhudi za serikali
za kuhakikisha watanzania wanakuwa katika maisha bora na ya uhakika.
Mbali na uzinduzi huo pia mgeni
rasmi huyo aliweza kuchangia Sh. milioni tano huku akiiwataka wadau na
taasisi zingine kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa na Taasisi ya
jana wajasiliamali na uwezeshaji (TEEYO).
kwaupande wake Murugenzi wa
taasisi hiyo Luhunga Ayubu alisema kwanza taasisi yake ina mwaka mmoja
tangua imeazishwa na imekuwa na mafanikio makubwa kwani hadi hivi sasa
inawachama hai zaidi ya 2000 na vikundi 132.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio
hayo taasisi inahitaji Sh.milioni 342 kwa ajili ya kuweza kutoa mikopo
kwa wananchama wake katika vikundi mbalimbali vya biashara.
“dhamira yetu ni kuona tuna
wainua wanachama wetu kibiashara pamoja na kuwapa elimu ya ujasialiamali
ili waweze kujimudu kimaisha na kupiga vita umasikini ambao umeonekana
kukithiri katika nchi yetu,’alisema Luhunga.
Akizungumzia malengo ya Taasisi
ni kuweza kuwasaidia wajasiliamali zaidi pamoja na kuanzisha mtandao wa
biashara kutoa uelewa binafsi ili kuepukana na magonjwa ambukizi.
No comments:
Post a Comment