Halmashauri
za Mkoa wa Njombe zimeagizwa kutenga maeneo ya kupanda miti kwa ajili
kusaidia vikundi vya Skauti vilivyopo katika Shule za Msingi na
Sekondari zilizopo katika Halmashuri zao.Pia wakuu wa Wilaya za katika
Mkoa huo wamegizwa kuwa walezi wa Skauti katika wilaya zao.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr.Rehema
Nchimbi leo tarehe 12 Januari 2015 aliyasema hayo kwenye sherehe ya
kusimikwa kuwa mlezi wa Skauti Mkoa wa Njombe .
Katika Sherehe hizo zilizofanyika Ikulu ndogo ya Njombe
,Dr.Rehema Nchimbi aliweza kuuwapisha Makamishna watano wa wilaya za
Makete,Ludewa,Njombe na Wanging’ombe.
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Skauti katika Mkoa wa Njombe kuwa
Mfano wa kuigwa katika masomo,nidhamu na kufanya kazi kwa umoja na
upendo katika maisha yao ya kila siku na kuwataka vijana wengine na
wazee kujiunga na Skauti kwani Skauti sio Jeshi bali ni vikundi
vilioundwa kwa utaratibu maalum kwa ajili ya kufundisha
Elimu,Upendo,nidhamu na mazoezi ya kukabiliana na maisha ya kila siku ya
Mwanadamu.
Sarah Dumba Mkuu wa wilaya ya Njombe alisema kuwa Skauti katika
Mkoa Njombe wamekuwa Msaada mkubwa katika matukio mbalimbali kama vile
maafa,sherehe na matukio mengine wamekuwa wametoa msaada mkubwa katika
matukio hayo.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Njombe Tutsiwene K.Mahenge amesema
kuwa kwa mkoa wa Njombe kunazaidi ya Skauti elfu tatu( 3000) ambao
waanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari na kusema kuwa skauti hao
huwa wanudhuria vipindi madarasani kama kawaida na skauti hao wanafanya
mazoezi siku za Jumamosi.
No comments:
Post a Comment