Meneja Chapa wa Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tigo Music( Tigo Kiboko Yako)
ambayo itawawezesha wasanii wa ndani kuweza kupata kipato kwa
kusikilizwa nyimbo zao kupitia simu za mkononi, pia itaambatana na
tamasha kubwa litakalofanyika tarehe 24 mwezi huu viwanja vya Leaders
Kinondoni. Msanii
Christian Bella akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali
wakati wa uzinduzi wa Tigo Music( Tigo Kiboko Yako) ambayo itawawezesha
wasanii wa ndani kuweza kupata kipato kwa kusikilizwa nyimbo zao kupitia
simu za mkononi, pia itaambatana na tamasha kubwa litakalofanyika
tarehe 24 mwezi huu viwanja vya Leaders Kinondoni. Ben Pol akitoa vionjo kwenye uzinduzi wa Tigo Music Kiboko Yao pembeni yake Wiliiam Mpinga (kulia) na Paulina Shao (kushoto)
Alli Kiba akiongea na wanahabari kwenye uzinduzi wa Tigo Music Kiboko
Yao pembeni yake Wiliiam Mpinga (kulia) na Paulina Shao (kushoto) Weusi nao watakuwepo, hapo wakitoa hamasa kwa fans wao wajitokeze kwa wingi kwenye Tamasha kubwa la Tigo Music.Diamond Platinum akiwashukuru Tigo kwa kuufungua mwaka vizuri mbele ya wanahabari na wasanii waliojitokeza kwenye mkutano. Mkubwa Fella na Yamoto Band wakizungumza katika mkutano huo.………………………………………………………………………………………
Tigo Tanzania imetangaza uzinduzi
wa Muziki wa Tigo ujulikanao kama “Tigo Music” kwa kushirikiana na
Deezer, ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha muziki itakayowapa
Watanzania muziki usiokuwa na kikomo.
Akizindua huduma hii mpya, Meneja
Chapa wa Tigo, William Mpinga, alisema kuanzia Januari 24, wateja wa
Tigo wenye vifurushi vya malipo ya kabla ya intaneti wana uwezo wa
kupata nyimbo milioni 36 za wasanii wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla
katika simu zao za mkononi za smartphone.
Vilevile, Tigo itatafuta miziki
mipya ya kusisimua ya wasanii wa ndani kupitia ushirikiano mpya na
kampuni ya Africa Music Rights, ambayo inawezesha, kutafuta na kusimamia
haki za muziki katika bara la Afrika, alisema Mpinga.
Kutakuwa na ghafla ya uzinduzi kwa
ajili ya Tigo Music katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam
tarehe 24 Januari ambapo wananchi watatumbuizwa na nyimbo tofauti
tofauti kutoka kwa wasaniii wa hapa nchini kama Diamond Platinum, Ali
Kiba, Professor J, Vanessa Mdee, Ben Paul, Isha Mashauzi, Malaika Band,
Khadija Kopa, Yamoto Band, Msondo, Sikinde na wengineo.
Juu ya kuwapa wateja wa Tigo
uwezekano wa kupata miziki ya kimataifa na ya hapa nchini bila kizuizi
chochote, Tigo Music, itawapa nafasi wasanii wa hapa nchini kujiongezea
kipato kutokana na nyimbo zao ambazo zitakuwa zimesikilizwa kupitia
huduma hii. Tigo itawapa wasanii hawa mafunzo ya jinsi ya kutumia na
kunufaika na huduma hii, alisema Bwana Mpinga.
“Kampuni ya Tigo Tanzania ni
kampuni iliyojengwa juu ya msingi imara wa ubunifu. Tunafurahia kuwa
kampuni ya kwanza ya mawasiliano Tanzania kuwapa wateja wetu muziki
usiokuwa na kikomo”.
“Kama bidhaa yenye maisha ya
kidijitali, lengo letu ni kuiwezesha tasnia ya muziki kwa kujenga jukwaa
ambalo si tu linaruhusu kupata nyimbo za wasanii wa ndani kwa urahisi,
lakini pia linawapa mafunzo wanamuziki wetu kwenye masuala muhimu kama
vile haki miliki na masoko. Hii ni njia yetu ya kusaidia vipaji vya
wasanii na kukuza tasnia ya muziki wa ndani, “aliongeza.
Tigo itaanzisha vifurushi
mbalimbali vya huduma ya muziki ambavyo vitawawezesha wateja wake
kuvipata moja kwa moja kupitia * 148 * 00 #.
Kuanzishwa kwa Muziki wa Tigo
(Tigo Music) nchini Tanzania kumetokana na mafanikio ya uzinduzi wake
nchini Ghana mwaka 2014 na Amerika ya Kusini mwaka 2012. Tangu
kuanzishwa kwake imekuwa ni sehemu muhimu kwa maisha ya kidijitali ya
watu ya kila siku na hii inaendana na matukio ya muziki wa ana kwa ana
yaliyowahi kufanywa na wanamuziki mashuhuri duniani, pamoja na yale
yaliyorekodiwa ndani ya studio.
Urushwaji wa muziki ni eneo
linalokua kwa haraka sana katika tasnia ya muziki kimataifa, na bidhaa
ya muziki tayari imekuwa ya pili kimaarufu kwenye vipengele vya simu za
mkononi katika Afrika.
No comments:
Post a Comment