Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akitoa taarifa ya kikao chama
kawaida cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika jana Ofisi kuu ya CCM
Kisiwandui jana mjini Zanzibar kwa waandishi wa habari hii. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
……………………………………………………………………………………………………..
Jana tarehe 13/01/2015 Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake
wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao chake cha kawaida cha
siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-
1. SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW
Chama Cha Mapinduzi
kimesikitishwa sana na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa muda mrefu
na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo:-,
i). Pamoja na yale ambayo
yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka serikali na vyombo
vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge juu ya swala hilo.
ii). Kamati Kuu imewataka wote
wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao, na
wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha.
iii). Aidha Kamati Kuu imeiagiza
Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa wale wote
waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la Escrow na wako
kwenye vikao vya maamuzi vya Chama. Kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili
kitafanyika tarehe 19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.
2. WALIOPEWA ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.
Itakumbukwa kuna makada sita wa
CCM walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye
mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa
adhabu zao mwezi wa pili mwaka 2015.
Baada ya muda wa adhabu zao
kuisha, itafanyika tathimini kuona kama walizingatia mashariti ya adhabu
zao. Na kama kuna ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu
zao wataongezewa adhabu.
3. SOKO LA MAHINDI
Kamati Kuu imepokea taarifa ya
mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya tathimini na uchambuzi,
pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati Kuu imeiagiza serikali
kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya Taifa ya Chakula (
NFRA)katika ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi wakulima badala ya
utaratibu wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha zaidi mawakala
badala ya wakulima moja kwa moja.
4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.
Kamati Kuu imepitisha ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.
Aidha ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa na vikao vijavyo vya Chama.
Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity
No comments:
Post a Comment