Meneja
wa Kitengo cha taarifa za Usalama wa Usafiri wa Anga, Bw. Deodore Mushi
akitoa maelezo ya namna ya mashine mbalimbali zinazotumika katika
chumba maalum cha kutolea taarifa za usafiri wa Anga zinavyofanya kazi,
kwa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea katika ofisi hizo
leo asubuhi kufanya tathimini ya utoaji wa huduma katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Wa Kwanza kulia ni Afisa
Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Biseko Chiganga (aliyevaa
koti jeusi), wa pili kushoto kwa Chiganga ni Afisa Usafirishaji, Bw
Benjamin Mbimbi na tatu kutoka kushoto ni Afisa Usafirishaji, Bw. Said
Marusu.
Meneja
wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo, akifafanua jambo kwa
wataalamu kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea kituo cha kuongozea
ndege leo asubuhi kufanya tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa
Anga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
Meneja
wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo akiwaonyesha wataalamu
kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi inayoonyesha aina ya ndege, mahali
inapokwenda na muda itakaotumia inakokwenda, katika kituo cha uongozaji
ndege kilichoko Katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere leo asubuhi
wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho. Meneja
wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo (mwenye kilemba
chekundu), akiwaelezaa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, namna
waongoza ndege wanavyotumia rada na kuelekeza marubani sehemu za kupita,
wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho leo asubuhi kufanya
tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa anga katika Uwanja wa
Ndege wa Julius Nyerere.
(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).
No comments:
Post a Comment