Taasisi ya WAMA Foundation imefanikiwa kupanua fursa za elimu kwa mtoto wa kike kwa mwaka 2014.
Hayo yamesemwa na Mke wa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete wakati Akiongea na
wenza wa mabalozi kutoka nchi mbalimbali katika ghafla fupi ya
kuukaribisha mwaka mpya 2015 iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam,
Mama Salma alisema kuwa baadhi ya
mafanikio yaliyofikiwa na Taasisi ya WAMA ni kukamilika kwa sekondari ya
WAMA Sharaf katika Manispaa ya Lindi.
“Ninayo furaha kuwataarifu kwamba
ujenzi wa shule ya sekondari ya WAMA Sharaf umekamilika, shule ambayo
itaongeza idadi ya wasichana wanaofaidika na WAMA” Alisema Mama Salma.
Aidha, aliitaja Shule ya Sekondari
ya Wasichana ya WAMA Nakayama kuwa sehemu ya mafanikio ya Tasisi hiyo
ambayo ina idadi ya wanafaunzi zaidi ya 400 na inatarajia kuchukua
wanafunzi 90 mwaka 2015, ambao ni yatima na wanaotoka kwenye mazingira
magumu.
Akiongelea kuhusu mafanikio
mengine Mama Salma alisema ni pamoja na kuimarisha afya ya mama
wajawazito na watoto ili kupunguza vifo, kupunguza mimba za utotoni, na
kupunguza kasi ya maambukizi ya HIV toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Mama Salma aliwashukuru wadau wote
wanaofanya kazi kwa kushirikiana na WAMA wakiwemo Mashirika yasiyo ya
Serikali kwa misaada na kuwaomba waendelee kushirikiana ili kutoa
mabadiliko chanya katika jamii husika.
Aidha, kwa niaba ya wenza wa
mabalozi waliohudhuria ghafla hiyo, Mke wa kiongozi wa mabalozi nchini
Bi Celine Mpango alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa juhudi anazofanya
katika kumkomboa mtoto wa kike na mwanamke kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment