Serikali ya Tanzania itaendelea
kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuendeleza ushirikiano na mahusiano mzuri
uliopo kati yake na nchi zinazounda umoja wa nchi za Ghuba (GCC).
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa
akifunga mkutano wa siku mbili wa wafanyabishara kutoka Tanzania na nchi za GCC
ambao ulianza Januari 15 hadi 16 mwaka huu.
Malima alisema kuwa Watanzania
umefika wakati wa kuboresha biashara zetu ili kuweza kuuza bidhaa bora ndani na
nje ya nchi na kukabiliana na changamoto za soko la kimataifa.
“Viwango vya mazao yetu
vinapaswa viewe bora, ambapo ubora huo utaruhusu bidhaa zetu ziuzike nchi
nyingine” alisema Malima.
Akitolea mfano, Malima
alisema Tanzania imejaliwa kuwa na mifugo mingi inayoweza kuzalisha nyama
ambayo soko lake tunalo tayari ambalo ni nchi za GCC na kusisitiza kuwa nyama
hiyo inapaswa kuandaliwa katika
machinjio salama na ya kimataifa ili kufungua fursa ya kuuza nyama hiyo maana
milango sasa ipo wazi kwa serikali ikishirikiana na wafanyabiashara nchini.
Kwa upande wake Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara kutoka nchi za Ghuba (FGCCC)
Abdulrahman Bin Saleh Al- Otainshan alisema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara wan
chi za Ghuba wameona na wanatarajia kufanya
biashara Tanzania katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo wanategemea kupata
mzao mbalimbali yanayohitajika nchi za Uarabuni.
Mazao hayo
yanayohitajika ni pamoja na mchele, matunda, mboga mboga, asali na nyama.Zaidi ya hayo, Rais hyo
wa FGCCC alisema kuwa nchi zianazounda umoja huo zinatarajia kuwekeza Tanzania katika
sekta za kilimo, mifugo, elimu, maji,
afya, ufundi na utalii.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
benki ya BADEA alisema kuwa Abdel Aziz Khelef alisema kuwa benki yake
itaendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na nchi
za GCC ambapo wamekuwa na uhusiano mzuri kwa zaidi ya miaka 40.
Nchi zinazounda umoja
wa GCC ni Kuwait, Oman, Bahrain, Qatar, UAE na Saud Arabia zinauhusiano wa
karibu na Tanzania kihistoria, lugha pamoja mila na desturi.
No comments:
Post a Comment